Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 27 February 2018

JAFO ATOA SIKU SABA HALMASHAURI ZIKAMILISHE MIPANGO KAZI YAO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sulemani Jafo ametoa siku saba kwa halmashauri zote nchini kukamilisha mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo michache itakayotekelezwa kwa asilimia 100.

Akizungumza leo mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kujadili mpango wa utekelezaji wa Miradi ya Fedha za Maendeleo za Serikali za Mitaa(LGDG) iliyoboreshwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na kushirikisha wakurugenzi, wenyeviti wa Halmashauri, maafisa mipango na makatibu tawala wasaidizi wa afya.

Alisema serikali inatarajia kutoa Sh bilioni 251 za maendeleo kwa ajili ya serikali za kipaumbele cha kwanza kikiwa ni afya iliyotengewa Sh bililioni 69.

Katibu Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mussa Iyombe akizungumza na kuwataka maafisa mipango kufanya kazi yao kwa kuzingatia taaluma na kuacha kuwa na nidhamu ya woga katika kuweka mipango katika halmashauri zao. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika Kikao kazi hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Kibakwe mkoani Dodoma na Waziri wa zamani wa TAMISEMI, George Simbachawene akisikiliza maelekezo ya Waziri Jafo.
 Baadhi ya wakurugenzi, wenyeviti wa Halmashauri, maafisa mipango na makatibu tawala wasaidizi wa afya wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment