Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 2 May 2017

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO MEI 2,2017

 Mbunge wa Bunda Mjini Esther Bulaya akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Nkuu, Sera, Bunge, Kzi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akijibu taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu shauri la kudharau Mamlaka ya spika linalowahusu wabunge, Freeman Mboiwe, Halima Mdee, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na wengine, Bungeni mjini Dodoma
 Spika wa Bunge Job Ndugai akihitimisha taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu shauri la kudharau Mamlaka ya spika linalowahusu wabunge, Freeman Mboiwe, Halima Mdee, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na wengine, Bungeni mjini Dodoma leo.Picha: Fadhili Akida- Daily News Tanzania Blog
 Mbunge wa Hanang, Dk Mary Nagu na Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga wakiwasili kwenye viwanja vya Bunge kuhudhuria kikao cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma
 Naibu Waziri wa wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Suleiman Jafo akijibu maswali ya wabunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu, Bungeni mjini Dodoma
Mbunge wa Geita Mjini, John Kanyasu akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma
 Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy Mohamed akifuatilia kwa makini mijadala ya Bunge, Bungeni mjini Dodoma
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangala akijadiliana jambo na Mbunge wa Segerea, Bonah Kaluwa wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.


MAKALLA AWAONGOZA MBEYA KUTWAA KOMBE LA AMANI 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ndiye Kocha Mchezaji wa Timu ya Viongozi wa Mkoa wa Mbeya akinyanyua juu kombe ka Amani, baada ya timu yake kuicharaza bila huruma timu ya viongozi wa dini Mkoa wa Mbeya kwa bao 4-1 katika Mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja Sokoine Mjini Mbeya siku ya Mei Mosi mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambae pia ni Kocha Mchezaji wa timu ya Viongozi wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akiwania mpira na Mchezaji wa timu ya viongozi wa dini, Pastory John wakati wa mchezo wa kuwania kombe la Amani 2017 uliopigwa katika uwanja wa sokoine mjini Mbeya juzi.  Viongozi wa Mkoa wa Mbeya walishinda kwa bao 4-1 na kutwaa kombe hilo. (Picha na Daily News Blog).

 Mtanange huo ukiendelea
 Kocha Mchezaji wa Timu ya Viongozi wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla 'akificha' mpira wakati wa mchezo huo.
 Makalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo.
 Mgenzi rasmi akisalimia timu zote mbili.
Mabingwa wa Kombe la Amani 2017 wakiwa na kombe lao.


Maadhimisho Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Yaanza Mwanza


Mtaalamu wa Mawasiliano nchini, Innocent Mungy akiwasilisha mada kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3.
Mkurugenzi wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini 'TMF', Ernest Sungura akiwasilisha mada kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Francis Nanai akichangia mada katika mkutano huo.
Mmiliki wa Kampuni ya Sahara Media Group, Antony Diallo akichangia hoja kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3.
Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akifuatilia mijadala mbalimbali kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3 linashirikisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.


Monday, 1 May 2017

SIKIA HAPA ALICHOKISEMA RAIS MAGUFULI KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI KITAIFA


RAIS MAGUFULI AAHIDI KUFANYA ANNUAL INCREMENT YA MSHAHARA NA PROMOSHENI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe Mosi Mei, 2017 amesema Serikali ya  Awamu ya tano imepanga kufanya  nyongeza ya kawaida ya kila mwaka katika mishahara yaani Annual increment, ambayo ilikuwa imesimama kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na promosheni.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo katika Sherehe za siku ya Wafanyakazi duniani zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema uamuzi wa Serikali wa kuanza kutoa promosheni unatokana na kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa Wafanyakazi hewa  zaidi ya wafanyakzi kumi 19,000 walibainika kuwa wafanyakazi  hewa.

''Yale mambo yote yaliyokuwa pending ikiwa ni pamoja na promosheni kwa sababu tulishindwa,  unaweza kupromoti mfanyakazi hewa hayupo,kwa sababu tungetoa promosheni wakati kuna wafanyakazi 19,000 hewa,maanake tungepromoti na 19,000 na siajabu na watu waliowaandika mule ndio wangeletwa katika mapendkezo ya promosheni'' amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewaonya watumishi ambao wamekuwa wakidanganya umri wa kustaafu ili waendelee kufanya kazi kwa muda mrefu na kuwa siku zao sasa zimekwisha.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amepiga marufuku uhamisho wa Wafanyakazi bila kuwalipa stahili zao kutokana na kuwepo na tabia ya kuwahamisha wafanyakazi bila kuzingatia taratibu hasa za malipo ya uhamisho.

''Sasa niwaombe wafanyakazi yeyote akihamishwa hakuna kuhama mpaka umelipwa pesa ya uhamisho,kuanzia juu mpaka chini,yeyote atakaye kuhamisha mwambie nipe hela yangu ya uhamisho ninapoenda akishindwa usihame kaa hapohapo ufanye kazi'' Amesema Rais Magufuli.

Amesema viongozi wengine wamekuwa wakiwahamisha wafanyakazi  kwa maslahi binafsi au visasi kutokana na maendeleo wanayowapata wafanyakzi
Rais Mgufuli amewahakikishia wafanyakazi kuwa Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kuwajali na kuwa  karibu nao katika kutimiza dhana ya utatu ya ushirikiano kati ya Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kwa lengo la kuleta maendeleo.

Aidha, Rais Magufuli amewaeleza wafanyakazi mipango mbalimbali anayofanywa na Serikali katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege mpya ,ujenzi wa Reli ya kisasa, utoaji elimu bila malipo na uboreshaji wa miundombinu katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika mkoa wa Kilimanjaro pia zimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ambapo kauli mbiu inasema,'' Uchumi wa Viwanda uzingatie kulinda Haki, Maslahi na Heshima ya Mfanyakazi''.


JIANDIKISHE SASA USHIRIKI DASANI MARATHON 2017, INAYOFANYIKA MAY 14, 2017


MKUU WA MKOA AOMBA USHIRIKIANO WA WAFANYAKAZI



Waalimu wa Shule mbali mbali za mkoani hapa wakiwa katika madhimisho ya Mei Mosi katika uwanja wa CCM Kirumba.
Wanafunzi wa shule ya ufundi ya Wavulana ya Bwiru wakiwa katika maadhimisho ya Mei Mosi katika uwanja wa CCM Kirumba
 *************
Na Alexander Sanga,Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amewaomba waajiri na waajiriwa wanahakikisha wanadumisha ushirikiano baina yao pamoja na serikali ili kuhakikisha wanaleta maendeleo nchini.

Akizungumza katika sherehe za kusherekea sikukuu ya Mei Mosi kimkoa iliyofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba katika wilaya ya Ilemela,Mongela alisema ushirikiano ukiwepo baina ya wafanyakazi utasaidia katika kutatua kero za wafanyakazi.

Mongela alikemea tabia ya wajiri kutoa hundi hewa wafanya bora pamoja na tabia ya ukopaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora wa Mei mosi uachwe haraka.

‘’Nakemea sana tabia hii ya kukopa zawadi za washindi wa wafanyakazi bora jambo sio zuri kabisa,mfano mzuri ni ofisi yangu wale wafanya kazi bora wa mwaka jana hawakupewa zawadi zao wamekuja kupewa zawadi za mwaka jana leo asubuhi(Jumatatu)’’ Mongela alisema.

Mkuu wa mkoa aliagiza zawadi za wafanyakazi bora wa wilaya ya Sengerema na Misungwi wapewe zawadi zao za mwaka jana.Pia alipongeza kauli mbiu ya Mei mosi mwaka huu inayosema ‘’Uchumi wa Viwanda,Ulenge Kulinda haki na maslahi na heshima ya mfanyakazi’’.

Kwa mujibu wa Mongela alisema kauli mbiu hii ni muafaka kabisa katika kutengeneza Tanzania ya viwanda ili kuendana na kasi ya Mheshimiwa rais John Magufuli.

Mongela aliziagiza Halmashauri na wilaya zote mkoani hapa zihakikishe zinakaa mabaraza ya wafanyakazi ili kuhakikisha zinatatua kero mbali mbali za wafanyakazi wake.Mongela alisema Halmashauri zote zikae vikao hivyo vya mabaraza kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

Mratibu mkuu wa Mei Mosi mwaka huu mkoani hapa Meshack Sarota ameomba makampuni ya mbali mbali mkoani hapa yaache mambo ya kuchelewesha mishahara kwa wafanyakazi wao.

Sarota alimuomba mkuu wa mkoa mkoa kuhakikisha anatatua kero mbali mbali za wafanyakazi mkoani hapa ili mkoa uweze kupata maendleo.

Sarota ameipongeza serikali kwa kuwalipa walimu posho zao pale wanapoahama kutoka shule mmoja kwenda nyingine.


RC MBEYA MAKALLA AONGOZA WAFANYAKAZI NA WANANCHI WA MKOA WA MBEYA KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI MKOA

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla leo ameongoza wafanyakazi wa mkoa wa Mbeya na Wananchi katika sherehe za wafanyakazi Mei Mosi mkoani humo.

Akizungumza baada ya kupokea maandamano ya wafanyakazi kutoka taasisi na kampuni mbalimbali mkoani humo Makalla alisema atahakikisha anashughulikia matatizo ya wafanykazi mkoani humo yaliyo katika ngazi ya mkoa na yale ya kisera atayawasilisha katika Wizara na Mamlaka husika kwa kutafutiwa ufumbuzi kwa wakati.

Asema serikali haitomuonea mfanyakazi yeyote katika uwajibishaji  kwa kumchukulia hatua za kinidhamu bali serikali itazingatia sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi.

Aidha Makalla amewataka waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa mujibu wa sheria.

Makalla amewakumbusha wafanyakazi pamoja na haki watimize wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii.

Pia amewashuruku Wafanyakazi, Viongozi wa wafanyakazi kwa kushirikiana n serikali katika kushughulikia changamotoza wafanyakazi.
 Wafanyakazi wakiandamana Mkoani Mbeya
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla pamoja na viopngozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya na wa Vyama vya wafanyakazi wakiimba wimbo wa mshikamano wa ndoa.
Mmoja wa wafanyakazi bora akikabidhiwa zawadi ya ufanyakazi bora.


TAZAMA VIDEO YA MAADHIMISHO YA MEI MOSI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Wafanyakazi wa MSD wakishirukia maandamano ya Wafanyakazi katika kuadhimisha Siku kuu ya Wafanyakazi Mei Mosi mkoa wa Dar es Salaam leo.
 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam wakiandamana katika maadhimisho ya Siku Kuu ya Wafanyakazi Mei Mosi Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo.


WAFANYAKAZI WA TSN WAUNGANA NA WENZAO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI

Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa Magazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo pamoja na Mitandao ya Kijamii ikiwepo Blog ya Dailynetzonline wakishiriki maandamano ya Mei Mosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa Magazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo pamoja na Mitandao ya Kijamii ikiwepo Blog ya Dailynetzonline wakishiriki maandamano ya Mei Mosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa Magazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo pamoja na Mitandao ya Kijamii ikiwepo Blog ya Dailynetzonline wakishiriki maandamano ya Mei Mosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na Kampuni Binafsi wakiandamana katika Siku ya Mei Mosi leo
 
 Wafanyakazi wa Bandari Dar es Salaam wakiandamana
 Wafanyakazi wa Chuo cha Usimamizi wa fedha wakipiga picha ya pamoja baada ya maandamano.
 Wafanyakazi wa Songas wakiwa uwanjani leo
 Wafanyakazi wakiandamana