Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday, 4 December 2017

MAMIA WAJITOKEZA KUSINDIKIZA MWILI WA MWANAFUNZI WA SCOLASTICA ALIYEUAWA

Msafara wa Magari ya waombolezaji na lililobeba mwili wa marehemu Humphrey Makundi ukipita eneo la Marangu mtoni wakati ukitoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuelekea kanisa la KKKT Usharika wa Mamba Kwa Makundi wilaya ya Moshi.
Ibada ya kumuombea marehemu Humphrey Makundi imefanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Kwa Makundi .
Ndugu ,Jamaa na Marafiki wakipita mbele ya jeneza kutoa Heshima zao za mwisho katka kanisa la KKKT Usharika wa Kwa Makundi.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akitoa heshima za mwisho katika ibada ya marehemu Humphrey Makundi.
Ndugu wakitoa heshima za mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira (wa pili toka kulia) akiwa na viongozi wengine wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Kilimanjaro akiwemo kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hami Issah (wa pili toka kushoto) wakishiriki ibada hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Humphrey Makundi.
Mkuu wa  Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Humphrey Makundi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimfariji Baba mzazi wa Humphrey,Bw Jackson Makundi
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimfariji, Mama mzazi wa Humphrey ,Bi Joyce Makundi.
Msaidizi wa Askofu ,Mchungaji Elingaya Saria akizungumza wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya Ndugu wa Marehemu wakifuatilia ibada hiyo.
Ndugu wa Marehemu wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Humphrey Makundi wakati ukipelekwa nyumbani kwao kwa ajili ya kuupumzisha katika nyumba yake ya milele.
Baba mzazi wa Humphrey akilia kwa uchungu wakati jeneza lenye mwili wa mwanae likiingizwa nyumbani kwao kijiji cha Mamba kwa Makundi wilaya ya Moshi .
Mama mzazi wa marehemu Humphrey Makundi ,Bi Joyce Makundi akilia kwa uchungu wakati jeneza lenye mwili wa mwanae lilipofikishwa nyumbani kwao kijiji cha Mamba kwa Makundi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu ,Humphrey Makundi likiingizwa kaburini .
Wadogo wa marehemu Humphrey wkiweka shada la maua katika kaburi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiweka shada la maua katika kaburi la Humphrey Makundi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,akijiandaa kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Humphrey.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia kaiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Humphrey Makundi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.


Friday, 1 December 2017

MAULID AL-NAWBI


MWILI WA MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA SCOLASTICA ALIYEUAWA KUZIKWA KWA MARA YA PILI JUMAMOSI


MWILI uliofukuliwa hivi karibuni kwa kibali cha mahakama kuondoa utata wa taarifa za kupotea kwa Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica, Humphrey Makundi(16) utazikwa kwa mara ya pili leo (Jumamosi ). 



Hatua ya kuzikwa kwa mwili huo uliokaa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa zaidi ya siku 14 sasa inatokana na kutoka kwa majibu ya sampuli ya vina saba (DNA) ikionyesha kuwa mwili ni wa Humphrey Makundi.



Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu Humphrey,Bw Jackson Makundi alisema mazishi yatafanyika katika kijiji cha Mamba kwa Makundi ,Marangu wilaya ya Moshi baada ya kupata kibali cha mahakama cha kuruhusu kuzikwa kwa mwili huo.



Makundi alisema shughuli za mazishi ya mwanae yataoongozwa na maaskofu wasaidizi kutoka Dayosisi ya Dodoma akiwemo mchungaji Samwel Mshana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) wakisaidiana na Askofu Msaidizi wa (KKKT) dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Elingaya Saria.




Novemba  6,mwaka huu taarifa za kutoweka kwa mwanafunzi huyo katika shule aliyokuwa akisoma ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo zilianza kuzagaa katika mitandao ya kijamii na baadae Novemba 7 mwaka huu mwili ulikutwa ukiwa umetelekezwa mto Ghona unaokadiliwa kuwa mita 300 kutoka katika shule hiyo.



Mwili huo ambao awali ulifikishwa katika Hosptali ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi ulipokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti na baadae kuzikwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi katika makaburi ya Karanga  kama mwili usiokuwa na ndugu.



Hata hivyo,baada ya kuwepo kwa taarifa ya kuzikwa kwa mwili huo ,familia ya Makundi iliomba kibali cha mahakama kuruhusu  kufukuliwa mwili huo kwa lengo la kujiridhisha ,mtu aliyezikwa kama kweli ni mzee kama taarifa za awali zilivyotolewa au ni ndugu yao. 



Tayari watuhumiwa  watatu kati ya 11 wanao shikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi huyo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa shtaka la mauaji .


Waliofikishwa mahakamani ni pamoja na anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Scolastica ,Edward Shayo , aliyekuwa mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha na Labani Nabiswa raia wa Kenya anayetajwa kuwa Mwalimu katika shule hiyo.


Mbele ya mahakama ya Hakimu mkazi ,Moshi ,upande wa Jamhuri katika shtaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi ,Julieti Mawore uliwakilishwa na Mwanasheria wa serikali Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea ,Faygrace Sadallah huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Eliakunda Kipoko anyemtetea Mshatakiwa wa pili katika shtaka hilo Edward Shayo.

Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo ,Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshtakiwa wa kwanza ,Hamis Chacha(28),wa pili Edward Shayo (63)  na wa tatu Laban Nabiswa (37) walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.


Kutokana na maelezo hayo Hakimu ,Mawore alieleza kuwa washtakuwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shtaka la mauaji huku akiwataka kungojea kufanya hivyo pindi watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata nafasi ya kuwasilisha mashahidi wao pamoja na kujitetea.


Kuhusu upelelezi wa Shtaka hilo Mwanasheria wa serikali Nassiri aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku akiwasilisha ombi la kupangwa tarehe nyingine kwa ajili kutajwa kwa shauri hilo wakati upelelezi ukikamilishwa.


Hakimu Mkazi ,Mawore aliahairisha shtaka hilo na kupanga kutajwa kwa shtaka hilo Desemba 8 mwaka huu  na  kwamba washtakiwa wote watarudishwa Rumande kutokana na  kesi hiyo kutokuwa na dhamana . Source: Dixon Busagaga-Moshi.


TLB KWIMBA WAHIMIZA UPANDAJI MITI

Mratibu wa chama cha wasioona wilayani Kwimba Isack Manumbu akipanda mti katika zahanati ya Malemve katika kata ya Igongwa.
****************
Na Alexander Sanga,Kwimba
Uongozi wa Chama cha wasioona wilayani hapa(TLB_Kwimba) imewahimiza wadau mbali mbali kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo yao ili kuepeka kujitokeza kwa tatizo la ukame.

Akizungumza katika zoezi la upandaji miti katika Zahanati ya Malemve kichopo kata ya Igongwa,Mratibu wa chama hicho Isack Manumbu alisema wameanza kupanda miti 300 katika zahanati hiyo ila bado chama chao kina mikakati ya kupanda miti zaidi wilayani hapo.

Kwa upande wake afisa mali asili wilayani Kwimba Joseph Swai alisema hali ya miti wilayani kwake sio nzuri kwakuwa kuna idadi kubwa ya ukataji miti kutoka kwa wakazi wa wilayani hapo.

Swai alisema kwa mwaka huo Halmashauri yao ina mikakati ya kupanda miti milioni 1,500,000/- katika kata zote 30 za wilayani hapo.

Joseph aliiomba pia serikali ipunguze bei ya gesi ili wananchi waache kukata miti kwajili ya kupata kuni.


CHINA YAAHIDI KUFADHILI UJENZI WA RELI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA (SGR)

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke,  wakiagana   baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao ambapo balozi huyo aliahidi kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kati nchi hizo mbili, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), wa tatu kulia akiwa katika mkutano na  Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke (wa pili kushoto) ambapo walikubaliana kuendeleza ushirikiano katika Biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande hizo mbili, mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
BALOZI wa China hapa nchini, Wang Ke, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kuahidi kuwa nchi yake iko tayari kushawishi taasisi za fedha ikiwemo Benki ya EXIM ya nchini humo kushiriki ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa baada ya kufanyika kwa upembuzi yakinifu wa mradi huo.

Alisema kuwa kutokana na ukubwa wa mradi huo, unaokadiriwa utagharimu Dola za Marekani bilioni 7.6 hadi kukamilika kwake, utahitaji kufanyiwa upembuzi yakinifu ili kukidhi masharti ya kupata mkopo kupitia Benki ya Exim na taasisi nyingine zitakazotaka kujenga mradi huo muhimu. 



65 WATEULIWA KUUNDA KAMATI NDOGONDOGO AFCON U17

Ukiacha Kamati Kuu ya kuratibu michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U17/2019) kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya uteuzi mwingine.

Uteuzi huo umeegemea zaidi kwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Maandalizi (LOC) wakiwamo viongozi wakuu wa TFF na wanafamilia wengine ambao kwa pamoja watafanya kazi ya kuandaa michuano hiyo itakayofanyika Tanzania mwaka 2019.

Wakati jina namba moja ni Mwenyekiti wa kila kamati ndogo wajumbe wengine katika kamati hizo ni kama ifuatavyo:

Miundombinu (Infrastructure)
  1. 1. Paul Makonda (Mwenyekiti)
  2. 2. Yusuph Singo
  3. 3. Sunday Kayuni
  4. 4. Leslie Liunda
  5. 5. Nassoro Idrissa
  6. 6. Mohamed Kiganja
  7. 7. Mhandisi Davis Shemangale
Masoko na Habari (Marketing, Commercial and Media) 



DK. MWAKYEMBE ANENA KILIMANJARO STARS IKISAFIRI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewaambia wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’, kuwa Tanzania inahitaji ushindi katika michuano ya Kombe la Baraza la Soka la Afrika Mashariki (CECAFA).

Dk. Mwakyembe aliyesema hayo jana Novemba 29, usiku wakati wa hafla ya chakula cha jioni ambako alitumia baraza hilo kuwaaga vijana hao akiwataka wachezaji wa timu hiyo kwenda Kenya kujitahidi.

“Msidharau mechi,” amesema Dk. Mwakyembe huku akisisitiza: “Tunataka ushindi. Mnakwenda Kenya kwa niaba ya Watanzania. Najua mmejiandaa vizuri kwa mazoezi maana siku hizi huwezi kushinda kwa kumtegemea (kuroga). Siku hizi mazoezi ni basic component.

Akasisitiza: “Nina matumaini makubwa nanyi. Nendeni na baraka zangu tele na kila anayekuja mbele yenu ni kumtandika tu. Tandika wote. KIla anayekuja piga tu maana mna kila kitu.” SOMA ZAIDI HAPA


SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika mjini Singida Novemba 30, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (mwenye miwani mbele) akiwa na wahitimu wenzake katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika mjini Singida, Novemba 30, 2017. 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akitelemka kutoka kwenye jukwaa baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili Katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera (Master of Education in Administration, Planning and Policy Studies) na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Waziri Mkuu MStaafu, Mizengo Pinda (kulia)  huku  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
***********
SERIKALI haijatoa ruhusa kwa Chuo Kikuu Huria (OUT) kiendelee kutoa kozi ya ‘Foundation’ kama ambavyo imedaiwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii.

Baadhi ya mitandao ilitoa taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho: “Waziri Mkuu aruhusu kozi za 'Foundation' Chuo Kikuu Huria” kwa madai kuwa alitoa ruhusa hiyo jana (Alhamisi, Novemba 30, 2017) wakati akiwa mkoani Singida ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu hicho.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Singida waliohudhuria mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Katoliki mjini Singida, Waziri Mkuu alisema Serikali bado inafanyia maboresho Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014.

“Kwa sasa Serikali inafanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo kwani sera tuliyonayo haifafanui vizuri jinsi ya kuwasaidia vijana wetu wajiendeleze kwa njia ya mfumo wa elimu huria na masafa,” alisema.

“Programu kama zilizoelezwa na Makamu Mkuu wa Chuo za Foundation, zinahitaji pia kufafanuliwa kwenye sera yetu, ambayo kwa sasa wataalamu wetu wanaendelea kuiboresha. Pindi itakapokamilika, tutaitolea taarifa kwa Chuo Kikuu Huria na wataalamu wataweza kushirikiana na sekta zote ili kuhakikisha jambo hili linakwenda vizuri,” alisema.

Mapema, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Tozo Bisanda alisema wamepokea barua kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwaarifu juu ya nia ya Serikali kutaka kurejeshwa kwa kozi za Foundation katika chuo hicho.

“Tayari tumekwisha wasilisha mtaala wa Foundation ulioboreshwa ili kukidhi matakwa ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), na tunasubiri mrejesho kutoka Kamisheni baada ya kikao chao, mapema mwezi ujao,” alisema Prof. Bisanda.


MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) UTAENDELEA KUTOA FIDIA BORA – ERIC SHITINDI KATIBU MKUU – OWM

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba ya kufunga Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia kilele leo alasiri kwenye Kituo cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha Novemba 30, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017. 
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Laure Kunenge, akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI. 


SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA 172

Na Alexander Sanga, DodomaWaziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa Seleman Jafo amesema serikali inaendelea na ujenzi wa vituo vya Afya 172 ambapo vinatarajia kukamilika tarehe 30 Desemba mwaka huu.

Akizungumza katika kipindi cha Tujadiliane kilichoandaliwa na umoja wa vilabu vya vyama vya waandishi wa habari nchini(UTPC),Jafo alisema serikali kila kituo tumepeleka milioni 500.

"Hii ni kwa mara ya katika historia ya nchi hii kujenga vituo vya Afya 172 ndani ya miezi minne na kila kituo tumepeleka milioni 500 tunajenga kliniki ya watoto,maabara,Mochuwari na Theatre" Jafo alisema.

Waziri Jafo alisema kila bado kuna tatizo kubwa sana la Afya na kwa sasa sera ya serikali ni kuhakikisha kila kijiji kiwe na kituo cha afya.

Akielezea kuhusiana na suala la sawa,Jafo alisema serikali imetenga bilioni 269 za bajeti ya sawa kwa mwaka huu wa fedha 2017/18.

Suleiman aliwapongeza wabunge wenzake kwa kusaidia kwenye ujenzi wa zahanati katika maeneo yao.

Jafo alisema suala la vyeti feki na watumishi hewa nilikuwa changamoto kubwa sana katika sekta ya afya lakini serikali mpaka sasa imepambana na kufanikiwa kuajiri watalamu wa afya 2058 katika maeneo mbali mbali nchini.

Katika sekta ya Elimu waziri Jafo alisema serikali itahakiksha inaajiri walimu 2700 kwa mwaka kwa shule za msingi na sekondari mpaka mwishoni mwa Disemba na pia alisema wanatarajia kuajiri walimu 11000 ambapo walimu wa shule ya msingi watakuwa 7000 na sekondari 4000.

Jafo alisema suala la mimba mashuleni bado ni kero kubwa sana na serikali mwezi Agosti ilitenga bilioni 16 kwajili ya ujenzi mabweni kwa shule 63 za sekondari nchini.


Friday, 24 November 2017

MBUNGE GAMA AFARIKI DUNIA

MBUNGE wa jimbo la Songea mjini, Leonidas Gama amefariki Dunia. 

Taarifa kutoka Songea zinasema kuwa Gama amefikwa na umauti usiku wa kuamkia leo mkoani Songea katika Hospitali ya Peramiho ambako alilazwa kwa muda mfupi kufuatia maradhi ya kiharusi ambayo yalimpata juzi usiku akiwa nyumbani kwake huko Likuyu nabaadae kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Gama amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.


Monday, 20 November 2017

IKULU YAKANUSHA KUTENGULIWA KATIBU MKUU UTUMISHI

Taarifa zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro sio za kweli na zipuuzwe.

Wananchi endeleeni kupokea taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi vya Serikali, na pia watumiaji wa mitandao ya kijamii mnakumbushwa kuwa kueneza taarifa za uongo ni makosa kisheria.

Serikali itawafuatilia wote waliozusha taarifa hizi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.


Friday, 17 November 2017

YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA WAKATI WA KUAHIRISHWA KWA BUNGE NOVEMBA 17, 2017

Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bunge, mjini Dodoma.

Mbungewa Viti Maalum, Hawa Mchafu Chakoma akiulizwa swali Bungeni, mjini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo akiuliza swali kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, mjin Dodoma.

Wabunge wakjadiliana wakati wa vikao vya Bunge, mjini Dodoma ambalo limeahirishwa leo. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


Wednesday, 15 November 2017

YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA NOVEMBA 15, 2017

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo wakati wa vikao vya Bunge, mjini Dodoma.
   Mbunge wa Viti maalum Tabora, Munde Tambwe akijadiliana na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson Bungeni, mjini Dodoma.
 Baadhi ya Wabunge wakijadiliana.

Baadhi ya wageni wakifuatilia vkao vya Bunge, mjini Dodoma. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


Monday, 13 November 2017

UKOSEFU WA AJIRA WAPUNGUA NCHINI

Na Katuma Masamba, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema,  ukosefu wa ajra kwa vijana nchini unazidi kupungua kutokana na juhudi mbalimbali za serkali. 

Amesema hatua hyo inatokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuboresha na kutengeza mazingira yatakayowawezesha vijana kujiajiri.

Mhagama ameyasema hayo wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/2018 ambapo alisema, tatizo la ajira ni changamoto ya kidunia lakini  serikali imekuwa ikijtahidi kuhakikisha inatengeza mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kuanzisha program 8rasisimishaji wa ajira ambazo  Urasimishaji Ujuzi kwa Vijana ambao wana ujuzi lakini hawakupitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya Ufundi.


MUHIMBILI KUANZA KUPANDIKIZA FIGO DESEMBA

Na Katuma Masamba, Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kabla ya Desemba 30, mwaka huu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) itaanza kutoa matibabu ya kupandikiza figo ikiwa ni hatua ya kupunguza wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi.

Ummy ameyasema hayo wakati akichangia Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018 ambapo amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakibeza juhudi mbalimbali za serkali katika kuboresha huduma za afya.

Amesema kwa sasa Hospitali ya Taifa Munimbili kupitia taasisi zake kwa kiasi kikubwa imepunguza wagonjwa waliokuwa wakipelekwa nje ya nchi. 

Amesema kipndi cha nyuma Hospitali ya Muhimbili ilikuwa ina uwezo wa kuwafanyia upasuaji watoto 15 kwa wiki lakini sasa hivi ina uwezo wa kuwafanyia watoto 50.