Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 4 May 2017

TEMEKE WAZAWADIA SHULE NA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Holycross, Prisca Muthoni kombe pamoja na cheti kwa shule hiyo kufanya vizuri katika elimu katika Manispaa ya Temeke. Makabidhiano hayo yalifanyika katika siku ya elimu ya Manispaa hiyo. (Picha na Mroki Mroki).
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jitegemee wakiimba wimbo maalum wa maadhimisho ya Siku ya Elimu Temeke.
Walimu kutoka Shule mbalimbali za msingi na Sekondari Manispaa ya Temeke wakiwa katika maadhimisho hayo Mei 4,2017.
Wanafunzi wenye ulemavu kutoka kituo cha Jeshi la Wokovu Dar es Salaam wanaounda kundi la Twaweza band wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya elimu Manispaa ya Temeke yaliyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha  Elimu  Dar es Salaam (DUCE), jana. (Picha na Mroki Mroki).
Wapiga ngoma wa Kundi la Tunaweza kutoka Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto Ally Rashidi , Nurdin Bilali na Jotham James  wakitoa burudani wakati wa Siku ya Elimu Manispaa ya Temeke iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jana.
Wanafunzi kutoka Sekondari ya Mbagala wakiigiza kama Askari wa kikoloni  katika vita vya Majimaji
IDARA ya Elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, imeomba kubadilisha baadhi ya shule za msingi ambazo zina wanafunzi wachache ziwe shule za sekondari kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi kujiunga kidato cha kwanza.

Shule hizo ni Ndalala yenye wanafunzi 332 na Serengeti yenye wanafunzi 361.

Ofisa Elimu Manispaa ya Temeke, Sylvia Mutasingwa alisema hayo jana kwenye maadhimisho ya Siku ya Elimu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo pia walitoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa shule zilizofanya vizuri pamoja na wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita.

Mutasingwa pia aliomba kuwatumia maofisa elimu kata ili kuwashirikisha wazazi kikamilifu katika suala la maendeleo ya elimu ya watoto wao.

Katika hatua nyingine, alieleza matatizo walinayo kuwa ni msongamano wa wanafunzi madarasani ukilinganisha na idadi ya vyumba vya madarasa vilivyopo.

Vile vile ushirikiano mdogo wa wazazi katika kupata taarifa za watoto wao kutoka kwa walimu pamoja na wanafunzi kutokufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao, mahudhurio na hata tabia za wanafunzi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi Felix Liyaniva, alisema amezipokea changamoto zote pia atashirikiana na wadau mbalimbali wa elimu katika kuzitafutia ufumbuzi.


MAKAMU WA RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA BODI YA MAKANDARASI MJINI DODOMA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
 Wajumbe  wa Mkutano wakimsikiliza kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Mhandisi Consolata Ngimbwa akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi  na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya  ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakandarasi Wanawake mara baada ya kufungua Mkutano wa siku mbili wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
****************


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani kwani wakandarasi hao watasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati anafungua mkutano wa siku Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi mwa mwaka 2017.

Makamu wa Rais amesisitiza wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na sheria pamoja na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na sio vinginenevyo.
Makamu wa Rais amewataka wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wanayopewa.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubuti kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira za kutosha kwa vijana wa Kitanzania.
“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje pekee ni lazima Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”
Kuhusu madeni ya wakandarasi, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Wakandarasi kuwa Serikali haijawasahau na bajeti ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambayo imepitishwa na bunge imezingatia kilio hicho cha Wakandarasi.

Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kuwa Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote inakuwa na ubora unaotakiwa.

Waziri Profesa Mbarawa amekiri kuwa kuna baadhi ya wakandasiri ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo hivyo kujenga miradi jinsi ya kiwango hivyo ni muhimu kwa wakandarasi hao kufanya kazi kwa ubora ili waweze kuaminiwa na Serikali na kupewa kazi.
Amesema kuwa Wizara yake itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakandarasi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.
Nae, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi Nchini Rhoben Nkori amesema bodi hiyo imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Usajili wa Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa bodi hiyo inawakandarasi 9,000 kote nchini.

Msajili huyo pia amesema kuwa katika kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi bodi hiyo ilikagua miradi 3,813 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 2714 sawa na asilimia 71.2 haikuwa na kasoro na miradi mingine ilikuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo miradi hiyo kutofanywa na wakandarasi waliosajiliwa na kutozingatia usalama wa wafanyakazi.
Kasoro nyingine ni wakandarasi kufanya kazi zaidi ya viwango vya madaraja yao,miradi kutosajiliwa na miradi kutokuwa na bango. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


KAJEMBE; MZARAMO ALIYEUTEKA MJI WA MOSHI KWA BIASHARA YA KUKAANGA MIHOGO

WAANDISHI wa Habari ni watu wa kuzunbuka sana nchini na Duniani kwa ujumla katika harakati za utafutaji habari za kuhabarisha jamii juu ya nini kimetokea wapi na kwanini kimetokea kama kina faida basi kitaweza kusaidia jamii nyingine inaposoma habari hiyo kwa kuelimisha, kuhabarisha au hata kuburudisha.

Februari 23,2012 Mpigapicha/Mwandishi wa Tovuti hii, Mroki Mroki alifika katika mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro na katika pitapita zake mtaani alibahatika kupita katika mtaa mmmoja maarufu na kukuta watu wengi wakisubiri kupaa huduma ya Mihogo ya kukaanga.

Hali ile na kwa jinsi alivyokuwa akiijua vyema Historia ya Mji wa Moshi na wachaga kwa ujumla juu ya ulaji wa mihogo ilimfanya nae aungane na watu wale kusubiri kupata kipande cha m,hogo wa kukaanga.

Wakati anasubiri alihamasika kuzungumza na mwendeshaji wa biashara hiyo na kukubaliana kuchukua taswira za biashara hiyo kuanzia maandalizi hadi ulaji wake huku wakiongea mawili matatu juu ya biashara hiyo.

Hakuna asiyejua kuwa wachaga walikuwa hawali mihogo kutokana na hapo zamani kula chakula hicho na watu kufa hivyo waliamini kuwa mihogo huwa na simu na si chakula kimfaacho binadamu kwa namna yeyote ile.

Lakini siku hizi hali ni tofauti katika Mji wa Moshi, kwani kila ifikapo jioni majira ya saa 10 hivi, baadhi ya wakazi wa Moshi wanakuwa katika haraka ya kwenda mahali kujipatia chakula wakipendacho. Chakula hiki kimetokea kuwavuta wengi sana ambao hata hapo awali walikuwa wakiamini yakwamba ulaji wa mihogo ni hatari sana.

Hofu hii ilitokana na baadhi ya wenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro hususani wachagga kuamini kuwa mihogo ni sumu na si chakula, lakini siku hizi mihogo inalika kwa wingi katika mji huu bila kuchagua kabila la mchagga, mpare, muarusha, mzungu ama anatoa Esia. 
Aliyefanikiwa kuwateka wakazi wa Moshi na kuwafanya kila ifikapo jioni wahahe kuitafuta Mihogo si mwingine bali ni Mzaramo Mzaliwa wa Chanika pale Kisumu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na hapa moshi anajulikana kama Mzee Kajembe. 
Nilipofika katika ofisi yake swali la kwanza kumuuliza kuwa “Mzee wewe ni mwenyeji wa wapi?” akiwa na tabasamu na pasi na shaka alinijibu kuwa mimi mwenyeji wa jiji la Dar es Salaam.
Kwajibu hilo, nikawa sina swali bali nilimpa hongera kwa kufanikiwa kuleta chakula cha Kizaramo mjini Moshi na kukiandaa vyema kiasi cha Mchagga kushindwa kulala bila kula kipande cha Mhogo kutoka kwa Kajembe.

Jinalake halini ni Rashid Nassor Kajembe, ananiambia kuwa aliingia mji wa Moshi akiyoka uzaramkoni mwaka 1982 na ilipofika mwaka 1984 akaamua kuanza kuuza mihogo ya kukaanga. 

Anasema mwanzo daima ni mgumu lakini sasa kidogo afadhali, maana anasema alipoanzia DSM Street miaka hiyo na bade katika mitaa ya Simu tofauti na sasa alipo New Street.

Kiukweli anawateja wa kila namna anasema Wahindi nao wanaila sana mihogo tena huifuata na kupanga foleni. Mhindi anasema “Walahi Ogo tamu kushinda Makate” Tupate matukio zaidi ya picha.
 Mihogo ikiwa jikoni katika eneo ambalo Mzee Kajembe anafanyia biashara Kajembe Shop.
 Kajembe akiwa na kijana wake Juma Kajembe wakimenya mihogo majira ya asubuhi.
  Mzee Kajembe akimenya mihogo hiyo
Wateja wa Mihogo ya Mzee Kajembe kama nilivyowaambia hapo awali kuwa ni wa kila aina na kila rika.
 Mmoja wa vijana wa Mzee Kajembe, Mohamed Ally akiweka mihogo jikoni


 Vijana hawapendi Chips mjini Moshi ni Mihogo tu kutoka kwa Mzee Kajembe. Mdau nakusihi ufikapo mjini Moshi usiache kufika New Street jirani na Hoteli maarufu za Zebra na Buffalo ujipatie Mihogo ya aina yake. Habari hii ilichapishwa mara ya kwanza na Fadher Kidevu Blog 2012.


Wednesday, 3 May 2017

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AONGOZA MAAZIMISHO YA SIKU YA UHURU WA HABARI ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipitia ratiba ya hafla ya Kongomano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wqa Vyombo Vya Habari Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar. 
Mc wa Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Ndg Suleiman Seif akitowa maelezo la kongamano hilo la kuadhimisha lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar.  
Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg Chande Omar akitowa maelezo wakati wa maadhimishi ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani ilioadhimishwa Zanzibar katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Kajubi Mukajanga akitowa maelezo wakati wa Kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar. 
Wageni waalikwa na Viongogozi wa Vyombo vya habari Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo. 
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Habari Tanzania Hassan Abdallah Mitawi akitowa maelezo ya hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutowa machache na kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhutubia Kongamano hilo la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud akitowa nasaha zake wakati wa kongamano hilo kabla ya kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhutubia hadhara hiyo ya waandishi wa habari mbalimbali walioko Zanzibar.


WANAFUNZI WAWILI WAFA KATIKA JALI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

WANAFUNZI wawili wamekufa hukubabiria wengine 24 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika enwo la Banda la Ngozi jijini Dar es Salaam leo. Anaandika Katuma Masamba.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema, ajali hiyo imetokea leo saa 12:30 asubuhi ambapo imehusisha lori aina ya Scania lenye namba T273 CEV na daladala aina ya Eicher lenye namba T376 DFT ambayo yaligongana uso kwa uso.

Kamishna Sirro amewataja wanafunzi waliokufa katika ajali hiyo ni Itlam Wema Athuman ambaye ni mwanafunzi wa Kidato cha kwanza shule ya Sekondary Msimbazi na Sakina Hamis Imamu mwanafunzi wa shule ya sekondari Mchikichini.

Amesema kati ya majeruhi 24 tisa ni wanawake na 15 ni wanaume na najeri 21 kati yao wamepata matibabu na kuruhusiwa.

Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari namba T.273 CEV scania  mali ya kampuni ya Mikoani Traders kuingia barabara ya pili bila kuchukua tahadhari kwa nia ya kuingia kwenye maegesho ya ofisi yao na kusababisha ajali hiyo.

Aidha alisema dereva wa lori hilo Isack Moshi amekamatwa kwa mahojiano zaidi na magari yote mawili yapo katika kituo cha Polisi Chang’ombe huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika hospitali ya  rufaa ya Temeke.


WANAFUNZI WAFANYA ONESHO KAMA LA MAKOMANDOO WA JWTZ


MAONYESHO YA SITA YA MADINI YA VITO YAANZA RASMI LEO JIJIJI ARUSHA

 Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akifatilia jambo wakati alipokuwa anazindua rasmi maonyesho ya sita ya vito na madini yanayofanyika katika hotel ya Mounti Meru ilipo jijini  Arusha(habari picha na Woinde Shizza,Arusha)

 baadhi ya madini yaliyoletwa katika maonyesho
 Meya wa jiji la Arusha naye aliuzuria katika uzinduzi wa maonyesho haya ya vito na madini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.