Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 4 May 2017

TEMEKE WAZAWADIA SHULE NA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Holycross, Prisca Muthoni kombe pamoja na cheti kwa shule hiyo kufanya vizuri katika elimu katika Manispaa ya Temeke. Makabidhiano hayo yalifanyika katika siku ya elimu ya Manispaa hiyo. (Picha na Mroki Mroki).
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jitegemee wakiimba wimbo maalum wa maadhimisho ya Siku ya Elimu Temeke.
Walimu kutoka Shule mbalimbali za msingi na Sekondari Manispaa ya Temeke wakiwa katika maadhimisho hayo Mei 4,2017.
Wanafunzi wenye ulemavu kutoka kituo cha Jeshi la Wokovu Dar es Salaam wanaounda kundi la Twaweza band wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya elimu Manispaa ya Temeke yaliyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha  Elimu  Dar es Salaam (DUCE), jana. (Picha na Mroki Mroki).
Wapiga ngoma wa Kundi la Tunaweza kutoka Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto Ally Rashidi , Nurdin Bilali na Jotham James  wakitoa burudani wakati wa Siku ya Elimu Manispaa ya Temeke iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jana.
Wanafunzi kutoka Sekondari ya Mbagala wakiigiza kama Askari wa kikoloni  katika vita vya Majimaji
IDARA ya Elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, imeomba kubadilisha baadhi ya shule za msingi ambazo zina wanafunzi wachache ziwe shule za sekondari kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi kujiunga kidato cha kwanza.

Shule hizo ni Ndalala yenye wanafunzi 332 na Serengeti yenye wanafunzi 361.

Ofisa Elimu Manispaa ya Temeke, Sylvia Mutasingwa alisema hayo jana kwenye maadhimisho ya Siku ya Elimu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo pia walitoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa shule zilizofanya vizuri pamoja na wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita.

Mutasingwa pia aliomba kuwatumia maofisa elimu kata ili kuwashirikisha wazazi kikamilifu katika suala la maendeleo ya elimu ya watoto wao.

Katika hatua nyingine, alieleza matatizo walinayo kuwa ni msongamano wa wanafunzi madarasani ukilinganisha na idadi ya vyumba vya madarasa vilivyopo.

Vile vile ushirikiano mdogo wa wazazi katika kupata taarifa za watoto wao kutoka kwa walimu pamoja na wanafunzi kutokufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao, mahudhurio na hata tabia za wanafunzi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi Felix Liyaniva, alisema amezipokea changamoto zote pia atashirikiana na wadau mbalimbali wa elimu katika kuzitafutia ufumbuzi.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment