Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday 12 January 2018

SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MAPINDUZI ZANZIBAR KATIKA PICHA

 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Heshma katika  sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani. 

 Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akipungia mkono wakati akiwasili katika uwanja wa Amani.

 Wanafunzi wakipita mbele ya jukwaa kuu katika maandamano ya sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.




 Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakiwa wamesimama  wakati gwaride la heshma(halionekani pichani) lilipokuwa likipita katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Mkapa akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Magufuli akipokea Saluti kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Magufuli akiagana na wanachi mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.

 Amiri Jeshi Mkuu na Rais  Dkt. John  Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar.

 Rais Dk John Magufuli akiondoka
Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani. 


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment