Rais
Dk John Magufuli leo Juni 22, 2017, amezindua barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata yenye urefu
wa Kilometa 64 na kuipongeza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
na wote waliofanikisha ujenzi wa barabara hiyo ambayo inasaidia kutatua
tatizo la msongamano wa magari katika barabara ya Chalinze – Dar es
Salaam na inapita katika eneo la Bagamoyo ambalo litajengwa bandari mpya
na eneo la viwanda.
Ujenzi wa barabara hiyo yenye madaraja makubwa matatu umegharimu Shilingi Bilioni 213 ikiwa ni fedha zilizotolewa na Serikali ya Tanzania.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya
Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu
chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga,
Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM
Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara
baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye
urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa
kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa
kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru
Kawambwa akisalimia kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata
yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani
Pwani
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TANROADS
Eng. Patrick Mfugale akizungumza kabla ya ufunguzi wa Barabara ya
Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu
chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng.
Patrick Mfugale akielezea hatua za ujenzi wa Madaraja katika barabara ya
Bagamoyo-Msata huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment