Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 22 June 2017

RUSHWA HUSABABISHA WANANCHI KUKOSA IMANI NA SERIKALI YAO: MAKAMU WA RAIS SAMIA

 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akihutubia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa zamani wa nchi ya Georgia, Mikheil Saakshvili akihutubia na kutoa uzoefu wa nchi yake dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia kitabu kinachoelezea mapambano dhidi ya rushwa na Rais wa zamani wa nchi ya Georgia, Mikheil Saakshvili (kushoto) wakati Ufunguzi Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
Washiriki mkutano huo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
Washiriki mkutano huo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
Wanahabari nao walishiriki mkutano huo wakifuatilia hotuba

Wabungewa Bunge la Tanzania nao walikuwepo katika mkutano huo.
********************
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema rushwa ni miongoni mwa vitu vinavyoharibu maendeleo na kwamba kukithiri kwa vitendo hivyo katika nyanja mbalimbali kunasababisha wananchi kukosa imani na serikali yao. Anaandika Katuma Masamba.



Samia ametoa kauli hiyo leo Juni 22,2017, wakati akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Kimataifa wa kubadilishana uzoefu katika vita dhidi ya rushwa ambapo amesema, rushwa inatakiwa kushughulikiwa kuanzia kwenye kiini na kwamba serikali inalihakikisha hilo.



“Rushwa ni uovu ambao umeendelea kuharibu nyanja zote za maendeleo ya binadamu. Rushwa hudhoofisha utawala wa sheria, hivyo huharibu uaminifu wa umma kwa serikali,” alisema Samia.



Alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imejidhatiti katika mapambano dfhidi ya rushwa na kwamba tayari kuna mikakati mbalimbali iliyowekwa kwa ajili ya vita hiyo ikiwemo Mkakati wa Taifa wa Kupambana na Rushwa na Mpango wa Utekelezaji wa Awamu ya Tatu (NACSAP III).



Aliongeza kuwa tayari mipango ya kuweka Sera ya Taifa ya Kupambana na Rushwa ambayo itagusa kila sekta inaendelea na kwamba lengo la mikakati huo ni kufanya mageuzi ya kiutawala katika sekta ya umma na binafsi,  kubadilisha tamaduni na mtazamo kwa wananchi na upatikanaji wa haki na ulinzi kwa watoa taarifa na mashahidi.



Malengo mengine ni kuongeza mapato ya serikali na kuongeza ubora wa bidhaa na huduma kwa wananchi  ili wawe na ari ya kulipa kodi  na kuhakikisha kwamba ofisi za serikali zinaaminika kwa wananchi kwa matendo na maamuzi kutokana na uwazi na wajibikaji kwa umma.



Mkutano huo unafanyika nchini kutokana na ombi la Rais John Magufuli kwa Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim kusaidia Tanzania katika kuimarisha utawala bora. Mkutano huo unaelezwa utakuwa msaada kwa Tanzania katika vita dhidi ya rushwa.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment