Mwanadada Suzan Michael 'Pretty Kind' aliyeimba limbo wa VIDUDUWASHA ambaye leo semrikali imemfungia kujihusisha na sanaa kwa miezi sita.
Na
Mwandishi wetu.
SERIKALI
imemfungia msanii Suzan Michael ‘Pretty Kind’ kujihusisha na sanaa kwa kipindi
cha miezi sita.
Akitangaza
uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema uamuzi huo ni kutokana na msanii huyo kutoa
wimbo wa “VIDUDUWASHA” aliyomshirikisha msanii mwenzake Gift Stanford ‘Gigy
Money, ambao haufuati maadili ya kitanzania.
Aidha msanii
huyo imebainika kuwa anafanya kazi ya Sanaa bila kusajiliwa na Baraza la Sanaa
la Taifa, pamoja na kuweka mtandaoni picha ya nusu utupu kinyume na maadili ya
Kitanzania.
“Kumekuwa
na wimbi kubwa la wasanii sasa hivi kutoa nyimbo zenye maneno ya matusi na
zisizo na maadili pamoja na wasanii hasa wanawake kupiga picha wakiwa wamevaa nusu
utupu na kuweka picha hizo katika mitandao,nataka kuwapa angalizo wasanii wenye
tabia hizi kuwa Serikali inawafuatilia kwa karibu na mwaka huu tumeanza na huyu
na wengine wanafuata,”alisema Shonza.
Miongoni
mwa wasanii ambao wametajwa kuwa miongoni mwa wanaokiuka maadili na kuchafua
sanaa ya Tanzania ni pamoja na mwana dada, Gift Stanford ‘Gigy Money’ na Jane Rimoy ‘Sanchi’ ambao nao wakati wowote
watakumbwa na mkono wa sharia.
Shonza amemtaka
msanii Gigy Money kufika ofisini kwake haraka, huku akionya kuwa msanii huyo
hawezi kushindana na Serikali.
Nae Katibu
Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Godfrey Mngereza amesema kwa mujibu wa Kanuni 31 (1) ya Baraza ya mwaka 2005,inaeleza kuwa
msanii kufanya kazi bila kusajiliwa ni kosa na anaweza kufungiwa, na pia kwa
upande wa mavazi zinasema msanii anatakiwa kuvaa mavazi yenye staha
yasiyomdhalilisha wala kudhalilisha watazamaji wake.
“Napenda
kuwasisitiza wasanii wote ambao wanajijua kuwa hawajasajiliwa BASATA kuja
kujisajili haraka na kwa wale waandaji wa kazi za Sanaa kama waongozaji , (Directors),Waandaaji
(Producers) na wamiliki wa Studio za kurekodi kazi za Sanaa ambao hawajasajiliwa nao waje kujisajili
haraka”, amesema Mngereza.
Msanii
Suzan Michael ‘Pretty Kind’ aliomba radhi mashabiki wake kwa kufanya makosa
hayo pamoja na watanzania wote kwa ujumla na kuaahidi kujirekebisha na kuto
kurudia tena makosa hayo.
Naibu
waziri Shonza ametoa rai kwa wamiliki wa
vyombo vya Habari kutokubali kupiga nyimbo au video za wasanii zisizo na
maadili kwani wanakuwa ni sehemu ya
kutangaza vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili kwani itafika mahali serikali itachukulia
hatua hata vyombo vinavyopiga nyimbo zisizo na maadili.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment