Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi akitoa
mada katika mkutano nchini Israel alipofanya ziara ya kutangaza vivutio
vya utalii vilivyopo Tanzania na fursa za biashara kupitia sekta hiyo.
Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta ushawishi kwa bodi ya
utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika sekta hii.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki akichangia
mada katika mkutano nchini Israel alipofanya ziara ya kutangaza vivutio
vya utalii vilivyopo Tanzania na fursa za biashara kupitia sekta hiyo.
Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta ushawishi kwa bodi ya
utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika sekta hii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake
jijini Dar es Salaam akitoa mrejesho kuhusiana na ziara yao iliyofanyika
nchini Israel ikiwa na lengo la kutangaza utalii wa Tanzania
iliyofanyika kuanzia Juni 11 hadi 15 mwaka huu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi(wapili
kushoto) katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Israel Job
Massima (wapili kulia) mara baada ya kumaliza mkutano uliowakutanisha
wadau wa sekta ya utalii wa nchini Israel kutambua fursa za utalii
zilizopo Tanzania. Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta
ushawishi kwa bodi ya utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika
sekta hii. Kulia ni Balozi mdogo wa Tanzania nchini Israel Kasbian
Chirich na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii
Dkt.Aloyce Nzuki. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
***************
Na Mwandishi wetu
BODI
ya Utalii Israel imeahidi kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
katika kutangaza vivutio vilivyopo na kukuza sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devota Mdachi,
aliyeongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.
Aloyce Nzuki, kuitembelea Israeli kwa siku tatu mwezi huu, amesema
ziara yao nchini Israel imeleta mafaikio katika sekta ya utalii
Tanzania.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukutana na wadau wa sekta ya utalii wakiwemo mawakala wa utalii na sekta ya malazi.
“Israel
imeonyesha shauku kubwa ya kushirikiana na sisi katika kuutangaza
utalii wa Tanzania. Mwaka jana tulipata watalii 22,000 kutoka nchini
humo ambapo wameahidi mwaka huu watakuja watalii wengi zaidi.
“Vilevile
kupitia vyombo vyao vya habari tumeeleza namna vivutio vyetu vilivyo na
mwonekano wa kipekee duniani, tumepokea maombi mengi ya kuja kutembelea
fukwe na hifadhi za wanyamapori.”
Alieleza
kuwa hifadhi zilizotajwa sana ni Katavi, Mahale, Ngorongoro na
Zanzibar: “Tunafahamu Waisraeli wanapenda kuangalia
wanyamapori.Nilipokuwa nikiwatajia wanayama tulio nao walionyesha
kufurahi hasa nilipowaeleza kuwa faru Fausta (55) mwenye umri mkubwa
kuliko wote barani Afrika yupo katika ardhi ya Tanzania walionyesha
kuvutiwa zaidi.”
Bw.
Nzuki aliuambia mkutano na wadau wa utalii nchini Israel katika Mji
waTel Aviv, : “Tanzania kuna fursa nyingi katika uwekezaji, upande wa
hoteli za kitalii. Ikiwa una kampuni ya kitalii pamoja nyumba ya wageni
ya kisasa unajiwekea uhakika wa kupata wageni wengi.
“Ukiwa
tayari unaweza kuja na kufuata utaratibu wa kisheria katika mamlaka
husika utapewa maelekezo. Tunawakaribisha kuwekeza katika utalii.”
Miongoni
mwa wawekezaji wanaofanya shughuli za kitalii nchini , Bwana Alon Hovev
anayemiliki kampuni ya utalii ya Sima Safari , ameuambia mkutano huo
kuwa sababu zilizomfanya kuwekeza Tanzania ni hali ya hewa na watu wake.
“Watanzania
ni wakarimu, nimevutiwa na mtindo wao wa maisha, vilevile kuna maeneo
mengi ya kuvutia ikiwemo pwani safi na mbuga za wanyama,” amesema Bw.
Hovev ambaye ameoa raia wa Tanzania.
Utalii
ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya mapato nchini, Waziri wa Maliasili
na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ameliambia bunge la bajeti hivi
karibuni na kueleza kuwa mwaka 2016 Tanzania ilipokea watalii milioni
1.2 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.9 mwaka 2015 walipokuja watalii
milioni 1.1.
Mwaka
jana sekta ya utalii iliingiza kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 2
ikiwa ni sawa na Sh Trilioni 4, mwaka 2015 iliingiza Dola bilioni 1.9.
Kiwango
hicho cha mapato kiliifanya sekta ya utalii kuchangia asilimia 17.5 ya
pato la taifa katika bajeti ya mwaka 2016/17 pamoja na kuingiza asilimia
25 ya fedha za kigeni.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment