Rais Dkt. John Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara
baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli akizungumza na wanahabari mara
baada ya kumaliza mazungumzo yake na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya
kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
**********
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Januari, 2018 amekutana na kufanya
mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Baada
ya mazungumzo hayo, Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kazi
nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa
ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika
maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s
Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambavyo vinazalisha
ajira nyingi kwa Watanzania.
“Nimepata
faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na
nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na
anahitaji kutiwa moyo.
“Moja
kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa
reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi
yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga
ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba
tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu
katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli
nakushukuru Mhe. Rais, you made my day” amesema
Lowassa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment