Mmoja
wa washiriki wa warsha ya wadau wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama
pori kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akichangia mada wakati wa warsha ya
kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya katika kukabiliana na magonjwa ya
milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba 16, 2017.
Mwakilishi
wa Shirika la DTRA kutoka nchini Marekani Bi. Jean Richard akizungumza na wadau
wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama pori wakati wa warsha ya
kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21) katika kukabiliana na
magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba 16, 2017.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mbazi Msuya (wa pili
kushoto)akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na wadau mbalimbali wa warsha
wadau wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama pori iliyokuwa ikijadili
Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21) katika kukabiliana na magonjwa ya
milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba 16, 2017. Wa pili kulia ni
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Ritha Njau.
Mwakilishi
wa Shirika la OIE katika nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw. Moetapele
Letshwenyo akizungumza na wadau wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama
pori wakati wa warsha ya kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21)
katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa
binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba
16, 2017.
Baadhi
ya washiriki wa warsha ya kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21)
katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa
binadamu wakifuatilia hotuba za Viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa
warsha hiyo iliyofanyika Jumatatu Oktoba
16, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mbazi Msuya akizungumza na wadau
wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama pori wakati wa warsha ya
kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21) katika kukabiliana na
magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba 16, 2017.
WashirIki
wa warsha ya kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21) katika
kukabiliana na magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu
wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa katika
Ofisi ya Waziri Mkuu, Mbazi Msuya mara baada ya kuzindua warsha hiyo Oktoba 16,
2017 Jijini Dar es Salaam.
*********************
SERIKALI imewataka
wadau wa sekta za afya ya binadamu, mifugo, wanyama pori na mazingira kuongeza
kasi ya ushirikiano na mashauriano ya pamoja ili kutekeleza vyema Mpango kazi
wa usalama wa afya unaolenga kudhibiti magonjwa yaambukizwayo na wanyama kwenda
kwa biandamu.
Hayo
yalisemwa jana (juzi) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa
Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mbazi Msuya wakati wa uzinduzi wa warsha ya
wadau za sekta za afya, mifugo, mazingira na wanyama pori waliyojadili Mpango
kazi wa Usalama wa Afya (2017-20) kupitia dhana ya Afya Moja.
Mbazi
alisema magonjwa yaambukizwayo na
wanyama kwenda kwa wanadamu yanachukua takribani asilimi 60-75 ya magonjwa yote
ya wanadamu, sambamba na kuleta athari kubwa kiuchumi, kiafya na kimaendeleo
katika ngazi zote,hivyo wadau wa afya hawana budi kutafuta mbinu mbadala za
namna ya kuyadhibiti na kuyatokomeza.
“Magonjwa
ya kichaa cha mbwa, ugonjwa wa malale, kimeta, home ya bonde la ufa na mengineyo
yameleta vifo kwa wanyama na wanadamu na hata ulemavu katika nyanja mbalimbali
hivyo ni wajibu wetu wataalamu wa afya tuyapatie pamoja na kupata ufumbuzi wa
kudumu kwa magonjwa haya” alisema Mbazi.
Aliongeza
kuwa Tanzania imeridhia na kutekeleza agenda ya usalama wa afya duniani mwaka
2014, hivyo katika kuweka msisitizo wa agenda hiyo, suala la afya moja limepewa
mkazo katika Nyanja mbalimbali ili kuweza kujiandaa na kujikinga na madhara
yatokanayo na matishio mbalimbali ikiwemo magonjwa ya milipuko ya binadamu na
wanyama.
Akifafanua
zaidi Mbazi alisema kupitia dhana ya afya moja, Serikali imeweka malengo ya
kuhakikisha kuwa sekta za afya ya binadamu, mifugo, wanyama pori na mazingira
zinashirikiana kudhibiti athari za magonjwa kama msingi mkuu wa kulinda afya ya
binadamu na wanyama.
Aliongeza
kuwa hadi sasa Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi chache zilizopiga
hatua nzuri katika kujipnaga na kuboresha mahusiano ya sekta za afya, mifugo na
utalii, na hivyo aliwataka wadau wa warsha hiyo kubaini changamoto zilizopo
ikiwemo kuboresha miundio iliyopo katika kukabiliana na majanga ili iweze kuwa
na manufaa zaidi.
Kwa
upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Ritha Njau
aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa uamuzi wa kuwakutanisha wadau wa sekta za
afya, mifugo, mazingira na wanyama pori kuwa ni hatua nzuri katika kukabiliana
na tishio la magonjwa ya milipuko yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Aliongeza
kuwa Mpango wa Serikali kuanzisha dhana ya Afya moja ni hatua mojawapo
inayodhirisha dhamira ya Tanzania katika kukabiliana na vimelea vya magonjwa ya
milipuko ya wanyama, juhudi ambazo katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa
zikiungwa mkono na WHO pamoja na mashirika na taasisi mbalimbali ya afya
duniani.
“Mwaka
2005 WHO ilianzisha kanuni maalum kwa nchi wanachama kuonyesha juhudi
mbalimbali ilizonazo katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko itokanayo na
wanyama na kuainisha vyanzo na asili ya magonjwa hayo” alisema Dkt Njau.
Naye
Mkurugenzi wa Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti wa Magonjwa wa milipuko katika
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dkt. Janeth Mghamba alisema
kupitia Mpango kazi huo, Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa madhara ya
magonjwa ya wanyama kwenda kwa binadamu yanatokomezwa nchini.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment