Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Grolius Luoga
akizungumza na watoto wakati wa kongamano la kuzuia mimba za utotoni kuelekea kilele
cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yatakayofanyika tarehe 11
Oktoba 2017 katika wilaya ya Tarime
mkoani Mara.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto,Magreth Mussai akiwasalimia watoto waliojumuika kwenye kongamano la kuwajengea
watoto uelewa wa kujilinda dhidi ya ndoa za utotoni siku moja kabla ya
maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Kitaifa yatakayofanyika tarehe 11
Oktoba, 2017 wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Mwakilishi wa watoto wilayani Tarime Anna
Simon akiwakilisha watoto wa wilaya ya Tarime kutoa salamu za watoto kwa,
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw. Glorius Luoga(hayupo pichani) wakati wa mjadala wa ulinzi wa
watoto katika ngazi ya familia, shuleni, mtaani na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya watoto, wazazi, walezi na wazee wa
mila katika wilaya ya Tarime wakifuatilia kwa makini nasaha za Mkuu wa Wilaya ya
Tarime, Grolius Luoga(hayupo pichani) kuhusu wajibu wa kuwalinda watoto
dhidi ya mimba za utotoni katika wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime,Grolius Luoga
akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa mwakilishi wa watoto Anna Simon mara baada
ya kufungua kongamano la watoto wilaya ya Tarime, mkaoni Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Grolius Luoga
akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa ulinzi na usalama wa mtoto katika
ngazi ya jamii wilaya ya Tarime, mkoani Maramara baada
ya kufungua kongamano la watoto.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment