BALOZI wa Tanzania nchini Uingereza,Dk. Asha-Rose Migiro ni miongoni mwa wajumbe 18, walioteuliwa na Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, watakaounda Bodi ya Ushauri ya
Masuala ya Upatanishi ya Umoja huo wa Mataifa.
Bodi hiyo, iliundwa hivi
karibuni baada ya Guterres kusikitishwa na matukio ya mauaji ya raia kutokana
na migogoro na vita inayoendelea katika nchi mbalimbali duniani.
Pamoja na Migiro, wajumbe
wengine walioteuliwa kuwemo katika bodi hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi
ya Graca Machel Graca Machel, Rais Mstaafu Olusegun Obasanjo, aliyekuwa Rais wa
Chile Michelle Bachelet na Mjumbe wa Baraza la Katiba Sri Lanka Radhika
Coomaraswamy.
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Programu ya Usalama, Wanawake na Amani katika chuo kikuu cha Columbia Leymah
Gbowee, Mjumbe wa Bodi ya Kimataifa ya Maafa Raden Mohammad Marty Natalegawa, Mjumbe
wa Klabu ya Madrid Roza Otunbayeva na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Knowledge
and Freedom (FOKAL) Michele Pierre-Louis.
Pamoja na wajumbe hao, wengine
ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya maafa Jean-Marie Guehenno, Mjumbe wa Baraza
la Wanawake viongozi Duniani Tarja Halonen, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Majadiliano ya Haki za Binadamu David Harland na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Taasisi ya Asia Noeleen Heyzer.
Wajumbe wengine ni Mjumbe wa Baraza
la Seneti ya Jordan Nasser Judeh, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje nchini Algeria
Ramtane Lamamra, Rais Mstaafu wa Timor-Leste Jose Manuel Ramos-Horta, aliyekuwa
Mwenyekiti wa watalaamu washauri wa UN kuhusu kujenga amani Gert Rosenthal na
Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment