Rais wa Uganda, Yoweri Museven akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Tanga jana tayari kuhudhuria sherehe za uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga. Marais John Magufuli na Rais Museven watashiriki katika uwekaji huo wa jiwe la msingi. (Picha na Mroki Mroki).
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na kupokewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika kesho katika eneo la Chongoleani mkoani Tanga.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara
baada ya kuwasili katika Ikulu ya Tanga kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi
la ujenzi wa mradi mkubwa wa
usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya
Tanga.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya
kuwasili katika Ikulu ya Tanga.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake wakati akielekea kwenye Dhifa ya
kitaifa aliyomwandalia Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Ikulu ya Tanga.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment