Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday, 4 August 2017

MAKONDA APOKEA VITANDA 150 VYA HOSPITALI NA MAGODORO YAKE KUTOKA AMSONS GROUP

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akijaribu moja ya vitanda 150 alivyopokea msaada kutoka  kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group iliyomua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Samaam Paul Makonda, (kulia) akipokea msaada  wa Vitanda 150 na magodoro 150 pamoja na mashuka vyenye dhamani ya shilingi milioni 300, kwa Meneja Biashara wa Kampuni ya Mafuta Camel Oil, Suleiman Amour. makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amepokea Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye tamani ya zaidi ya shilingi Million 300 kutoka kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group iliyomua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.

Akizungumza baada ya kupokea Vitanda hivyo, Makonda amesema amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

“Sitaacha kutafuta kwaajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ili mradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri ili siku moja waone kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Magufuli, sisi tunataka Maendeleo na sio Siasa ndio maana hivi vitu vyote tunavyofanya vinatumiwa pia na wapinzani” Alisema Makonda.

Makonda amesema anatamani siku moja kila mama anaekwenda kujifungua alale kitanda kimoja mwenywe na sio kama ilivyo sasa ambapo wanatumia kitanda kimoja kinamama watatu hadi wanne.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment