Kampeni
za wagombea mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika
shirikisho, zinaendelea.
Kwa
mujibu wa kanuni 11.10 ya uchagizi wa TFF, kampeni hizo za wiki moja
hadi Ijumaa wiki hii ambako Uchaguzi Mkuu utafanyika Agosti 12, mwaka
huu kwenye Ukumbi wa Hosteli ya Mtakatifu Gasper mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa kamati hiyo iliyokutana Jumamosi Agosti 5 2017, wagombea ambao wanawania urais ni pamoja na Wallace Karia, Imani Madega, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayay, Shija Richard na Emmanuel Kimbe.
Katika nafasi ya Makamu wa Rais wanaowania ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
Kanda
namba 1 ya Mikoa ya Kagera na Geita: waliopitishwa ni Saloum Chama,
Leopold Mukebezi na Kaliro Samson wakati Kanda namba 2 inayounganisha
mikoa ya Mara na Mwanza wamo Aaron Nyanda, Vedastus Lufano, Samwel
Daniel na Ephraim Majinge.
Kanda
namba 3 (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu) wanaowania nafasi hiyo ni
Stanslaus Nyongo, Bannista Rogora na Mbasha Matutu ilihali Kanda namba 4
(Mikoa ya Arusha na Manyara) waliopitishwa ni Omar Walii, Sarah Chao na
Peter Temu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Katika
Kanda namba 5 inayounganisha mikoa ya Kigoma na Tabora waliopitishwa ni
John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael wakati
Kenneth Pesambili na Baraka Mazengo – wote wamepitishwa kuwania ujumbe
kupitia Kanda namba 6 yenye mikoa ya Katavi na Rukwa.
Kanda
namba 7 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa waliopitishwa ni Elias
Mwanjala, Cyprian Kuyava na Erick Ambakisye huku Kanda namba 8 yenye
mikoa ya Njombe na Ruvuma waliopitishwa ni James Mhagama, Golden Sanga,
Vicent Majili na Yono Kevela.
Kanda
namba 9 Lindi na Mtwara Athumani Kambi na Dunstan Mkundi (wamepitishwa)
wakati Kanda namba 10 Dodoma na Singida waliopitishwa ni Hussein
Mwamba, Steward Masima, Ally Suru na George Komba.
Kanda
namba 11, mikoa ya Pwani na Morogoro waliopitishwa ni Charles
Mwakambaya, Gabriel Mkwawe na Francis Ndulane wakati Kanda namba 12
Kilimanjaro na Tanga waliopitishwa ni Khalid Mohamed na Godluck Moshi.
Kanda
namba 13 Dar es Salaam: waliopitishwa ni Emmanuel Kazimoto, Abdul
Sauko, Ayoub Nyenzi, Shaffi Dauda, Peter Mhinzi, Lameck Nyambaya, Mussa
Kissoky, Said Tully, Ally Kamtande, Aziz Khalfan, Ramadhani Nassib na
Saad Kawemba.
Hii
sasa ni orodha ya mwisho baada ya baadhi ya wagombea kufanikiwa
kushinda rufaa zao katika Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakipinga
kuondolewa na Kamati ya Uchaguzi.
Kamati
ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) na kueleza kuwa iliwakamata viongozi wa soka kutoka
mikoa mbalimbali katika mazingira ya kuvunja sheria za nchi na kanuni za
uchaguzi.
Kamati
iliamua kuwaondoa wagombea hao ambao ni Shafii Dauda wa Dar es Salaam;
Banista Rugora wa Shinyanga; Ephraim Majinge wa Mara na Elias Mwanjala
wa Mbeya katika kuwania nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika
uchaguzi ujao wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu kwa
ukikwaji wa Kanuni ya 14 (3) inayozungumzia kampeni kabla ya wakati.
MAJIBU KAMATI YA RUFAA ZA UCHAGUZI
Kamati
ya Rufaa za Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania pia
imetoa matokeo ya rufaa nne ilizosikiliza Jumamosi Agosti 5, 2017
zilizokatwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi katika mchakato wa kuwania
nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TFF.
kamati hiyo. Majibu hayo, yalitoka Kamati ya Rufaa. Warufani walipinga kuondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi.
Waliokata Rufaa ni Fredrick Masolwa ambaye
awali hakupitishwa kuwania nafasi ya urais kwa kukosa uzoefu kwa mujibu
wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za uchaguzi za TFF. Kamati ya Rufaa
ilitupilia mbali hoja hiyo kwa sababu ya rufaa kukosa kigezo cha
kutolipia kwa mujibu wa katiba ya TFF.
Mwingine
ni Mgombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Kanda namba 7 (Mikoa ya Mbeya
na Iringa), Abdusuphyan Sillah awali hakupitishwa kwa kukosa uzoefu kwa
mujibu wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za uchaguzi za TFF.
Rufaa
yake ilikuwa na vigezo, lakini ilikosa hoja za uadilifu kwa mujibu wa
Kanuni ya 9 (7) kwani mrufani alikosa uadilifu kwa kutoa taarifa za
uongo mbele ya kamati.
Kanda
namba 11 (Mikoa ya Pwani na Morogoro), Hassan Othuman awali
hajapitishwa kwa kukosa uadilifu jambo ambalo alilikatia rufaa Kamati ya
Rufaa ya Uchaguzi ya TFF. Hata hivyo, alituma ujumbe mbele ya Kamati ya
Rufaa akitangaza kujitoa.
Kanda
namba 13 Dar es Salaam: Saleh Abdallah awali hakupitishwa kwa kukosa
uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za uchaguzi za TFF.
Kamati ilitupilia mbali rufaa yake kwa sababu kwanza hakulipia hivyo
kukosa vigezo pia hata mrufani mwenyewe hakutokea kutetea rufaa yake.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment