NAIBU Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani
amewahimiza watanzania kutumia kikoa(domain) ya tz jambo ambalo
litachangia ukuaji wa uchumi. Anaandika Anastazia Anyimika.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa la watoa huduma za mitandao wa
intaneti kwa Afrika ambao tanzania ni mwenyeji alisema kwa sasa Tanzania
iko nyuma sana kwa kuwa na rajisi ya watumiaji 14,000 kati ya
watanzania mililoni 45.
Alisema kwa watanzania kujiunga na kikoa (.Tz) kutaisadia wafanyabishara na wajasiliamali kufanya biashara zao na kukuza uchumi wa nchi.
Alisema kutokana na uchache wa watumiaji lunaifanya serikali kutoa ruzugu ya kuendesha kikoa hicho na kuwa jinsi watu wengi wanavyojiunga, ndipo gharama za wanaojiunga zinaweza kupungua.
Aidha, Ngonyani alisema kwa sasa gharama za interneti
zimepungua kwa asilimia 50 baada ya kukamilika mkonga wa taifa wa
mawasiliano.
Naye Makamu wa Rais wa taasisi ya Afrika ya kikoa(Africa
Top Level Domains organisation-AfTLD) Ali Hadji Mmadi alisema kwa sasa
Afrika inawatumiaji miloni 2.9 kati ya wananchi bilioni moja wa bara
hili.
"Miaka ya nyuma watumiaji wa domain walikuwa mililoni moja
na wamepanda hadi kufikia mililoni 2.9, idadi hii ni ndogo ukilinganisha
na idadi ya watu," alisema.
Naye Meneja Maendeleo wa Afrika, Michuki Mwangi alisisitiza
kila wananchi katika nchi za Afrika kutumia kikoa chao na kuwa na sera
rafiki za kuwaongoza watumiaji wa interneti.
Mwenyekiti wa Watoa huduma za Intaneti nchini Tanzania (TISPA), Erik Rowberg akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo na kuwahimiza watanzania kutumia kikoa cha tz kwani ni kitambulisho peke cha utaifa wao kwani hata yeye anajivunia kutumia kikoa hicho cha .tz katika tovuti yake ya www.habari.co.tz.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo la tano la
Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA), Dkt, Raynold Mtungahema akizungumza wakati wa ufunguzi huo.
Washiriki wakifuatilia mkutano huo.
NAIBU Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani akizungumza wakati akifafanua jambo kwa wanahabari.
Waratimu wa Mkutano huo wakizungumza na waandishi wa habari.
Mijadala mbalimbali ikiendelea.
washiriki wakifuatilia mijadala
Mijadala ikiendelea ...
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani(walioketi katikati) na waratibu wa kongamano hilo kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment