MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde leo amekabidhi mabomba ya kusambazia maji kwa wananchi wa jimbo lake ambao aliwaahidi kufanya hivyo katika harakati za kutatua kero ya maji jimboni kwake.
Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akikabidhi mambo hayo.
Wananchi wakimshukuru Mbunge wao.
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, leo amekamilisha ahadi yake katika kijiji cha Matumbulu kwa kutoa mabomba ya kutandazia maji kijiji kizima yenye urefu wa Km 1 na yenye thamani ya zaidi ya Tshs 8m.
Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo wananchi hao walipigwa na duwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo kubwa la kijiji ilikuwa ni changamoto kubwa na iliyodumu mrefu hali iliyopelekea wananchi kutumia maji ambayo si safi na salama.
Wananchi wengi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.
Akizungumza katika tukio hilo, Mavunde amesema"Ni matumaini yangu kwamba ile adha kubwa ya upatikanaji wa wa maji katika eneo kubwa la kijijini Matumbulu itaisha na kusaidia wanakijiji kupata maji safi na salama kwa wakati"
Aidha Diwani wa kata hiyo, Emmanuel Chibago amempongeza Mbunge Mavunde kwa anavyojitoa kuwatumikia wanadodoma na kuwaletea maendeleo na hivyo kuwaomba wanadodoma wampe ushirikiano ili afanye makubwa zaidi

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment