Spika Mstaafu wa Bunge na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya
Taifa (NHIF), Anne Makinda akimkabidhi kadi ya Bima ya Afya ya Toto Kadi mmoja wa watoto aliyekatika huduma hiyo na wazazi wake.
Spika Mstaafu wa Bunge na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya
Taifa (NHIF), Anne Makinda (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa
Meneja wanachama wa NHIF, Elentruda Mbogoro, wakati Mwenyekiti huyo
alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es
Salaam (DITF) yanayofanyika viwanja vya Mwl. Julis K Nyerere, Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Anne
Makinda ameiomba serikali kutoa agizo kwa wanafunzi wanaokwenda
shule za bweni kuwa na bima ya afya, ili kupunguza gharama
kwa wazazi pindi wanapougua wakiwa masomoni. Anaandika Katuma Masamba.
Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge Mstaafu ametoa ombi
hilo katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa (DITF) yanayofanyika
katika viwanja vya Mwalimu Julius K Nyerere, barabara ya Kilwa jijini
Dar es Salaam.
Amesema licha ya wazazi kutakiwa kulipia gharama za
matibabu kwa mtoto wake wakati anapojiunga na shule, lakini mtoto huyo
anapoumwa akiwa masomo hulazimika kurudishwa nyumbani ambapo mzazi
huingia gharama za matibabu.
"Shule zote zinapokuwa zimechagua wanafunzi wa kujiunga na
shule zao huwa zina maelekezo, ikiwa in pamoja na kila mzazi kuchangia
matibabu ya mtoto wake shuleni".
"Serikali ingetoa amri katika suala la bima ya afya kwa
kila mwanafunzi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma. Unajua inauma
sana mzazi unalipa hela ya matibabu lakini mtoto akiumwa unapigiwa simu
umfate," amesema Makinda.
Amesema kama serikali itatoa amri ya wanafunzi kuwa na bima
ya afya itawawezesha wazazi kuwa na uhakika wa afya za watoto aao hata
kama wataugua wakiwa safarini watapata huduma za matibabu katika vituo
vya afya na hospitali mbalimbali nchini.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment