Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 27 June 2017

SHEIKH ALHAD; AFANYAYO RAIS MAGUFULI YANAENDANA NA MAFUNDISHO YA DINI YA KIISLAMU

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli za kulinda rasilimali za taifa zinaenda sawa na mafundisho ya dini ya kiislamu.


Alhad ameyasema hayo leo (Jumatatu) wakati akitoa hutuba baada ya swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Amesema katika mafundisho ya dini ya kiislamu kuchezea rasilimali ni haramu, hivyo Waislamu na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuunga mkono jitihada hizo za kulinda rasilimali za taifa.

"Jitihada anazofanya Rais wetu ni sawa kabisa na mafundisho ya dini yetu ya Kiislamu, anachofanya ni kulinda keki ya taifa ili kila mmoja anufaike na keki hiyo, hili ni jambo zuri," amesema Sheikh Alhad.

Aidha, amewataka waislamu kuitumia sikukuu ya leo kuliombea taifa amani na kuwaombea viongozi wote ili waweze kutekeleza yaliyo mema kwa ajili ya Watanzania wote.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment