KUFUATIA Kifo
cha Shabiki maarufu wa Klabu ya Yanga, Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Chama cha
Mapinduzi (CCM) Ali Yanga, Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa
wote waliofikwa na msiba huo.
Rais Magufuli
ametma salamu hizo leo kwa familia ya marehemu, wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), uongozi wa Klabu ya Yanga na wanamichezo wote kwa ujumla
kufuatia kifo cha shabiki mkubwa wa timu ya Yanga Ali Mohamed maarufu kwa jina la Ali Yanga.
Ali Yanga
amefariki dunia jana jana Juni 20, 2017 kwa ajali ya gari iliyotokea katika
Kijiji cha Chipogolo kilichopo katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Rais Magufuli
atamkumbuka Ali Yanga kwa uzalendo wake na mchango wake wa kuhamasisha na kushabikia
masuala mbalimbali ya kitaifa na hasa michezo, ikiwemo kuishabikia timu yake ya
Yanga, timu ya soka ya Taifa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na shughuli za
kiserikali kama vile Mwenge wa Uhuru na ziara za viongozi.
“Nimeguswa sana
na kifo cha Ali Yanga, nilikuwa nae wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015 ambapo alitoa mchango mkubwa katika uhamasishaji wa wananchi kukipigia
kura chama changu cha CCM, na pia amekuwa akiongoza mashabiki wenzake
kuishabikia timu ya Yanga na timu ya Taifa bila kuchoka. Kwa kweli alikuwa
hodari sana katika ushabiki wake.
“Natoa pole
nyingi sana kwa familia yake, viongozi wa timu ya Yanga, wanamichezo wote, wana
CCM na wote walioguswa na kifo cha Ali Yanga na namuombea kwa Mwenyezi Mungu
aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina” amesema Rais Magufuli.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment