BALOZI wa Tanzania nchini
Brazili, Dk. Emmanuel Nchimbi amewasilisha hati ya uteuzi wake kuwa Balozi wa
Tanzania Nchini Brazil, kwa Rais wa nchi hiyo, Michel Temer. Anaandika Mroki Mroki.
Balozi Dk Nchimbi
alisuindikizwa na maofisa kadhaa wa ubalozi wakati wa kukabidhi hati hiyo.
Itakumbukwa kuwa Dk. Nchimbi aliteuliwa na Rais,
Dkt. John Pombe Magufuli, mnamo Desemba 3, 2016 kuwa Balozi, ambapo katika
uteuzi huo jumla ya Mabalozi 15 waliteuliwa.
Mwezi Januari mwaka huu Rais Magufuli
aliwapangia kazi mabalozi wapya saba kati ya Mabalozi 15 aliyowateuwa kujaza nafasi
zilizo wazi katika Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali.
Miongoni mwa Mabalozi hao wapya waliopangiwa
vituo vya kazi ni pamoja na Balozi Mbelwa Brighton Kairuki wa Tanzania Beijing
– China China, Balozi George Kahema Madafa wa Tanzania Rome–Italy na Balozi
Emanuel John Nchimbi wa Tanzania Brasilia – Brazil.
Wengine katika Orodha hiyo alikuwepo, Balozi
Fatma Rajabu wa Tanzania Doha – Qatar, Balozi Prof. Elizabeth Kiondo wa Tanzania Ankara – Uturuki na Balozi Dkt.
James Alex Msekela wa Tanzania Geneva –
Umoja wa Mataifa.
Balozi wa Tanzania nchini
Brazili, Dk. Emmanuel Nchimbi aakisalimiana na Rais Brazil Michel Temer.
Balozi Dk Nchimbi akiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa Brazil na maofisa wa pande hizo mbili wakati wa kuwasilisha hati ya uteuzi kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment