Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday 31 May 2017

RAIS MAGUFULI AMLILIA MZEE NDESAMBURO



Marehemu Mzee Philemon Ndesamburo (kulia) akiwa na Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea wakizungumza jambo wakati wa Mkutano baraza Kuu la Chadema uliofanyika mjini Dodoma Mei 27,2017. 

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu”

Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho.

Mhe. Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.

Mhe. Dkt. Magufuli ameitaka familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo na wote waliguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu na amemuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi, Amina.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment