Home
About Us
Siasa
Uchumi
Biashara
Michezo
Burudani
Wasiliana Nasi
Have you got a good story?
Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.
Have you got a good story?
Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.
Saturday, 6 May 2017
NEC YATOA UFAFANUZI UTARATIBU WA KUMPATA MBUNGE NA DIWANI VITI MAALUM
Saturday, May 06, 2017
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa nafasi za Wabunge wa Viti Maalum wanaoteuliwa zipo kwa mujibu wa Sheria na zimeainishwa katika Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba inaeleza utaratibu mzima wa kuwapata Wabunge wanawake wa Viti maalum.
Amesema kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za wabunge kitapata Wabunge wa Viti Maalum kulingana na Kura ambazo chama husika kimepata.
Amefafanua kuwa Chama kinachopata asilimia 5 ya Kura zote halali za Wabunge katika Uchaguzi Mkuu kinatakiwa kuwasilisha orodha ya wanachama wanaopendekezwa kuwa wagombea wa Viti Maalum ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Aidha, ameeleza kuwa endapo inatokea nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali, Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyekiti wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume hukiandikia barua chama husika kukitaarifu juu ya uwepo wa nafasi wazi ya viti maalum ili kiweze kuwasilisha pendekezo la jina katika orodha kiliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015, ikiambatanishwa na Fomu namba 8 D ya kuomba jina lililopendekezwa liteuliwe na Tume katika nafasi ya Ubunge kulingana na sifa zilizoainishwa kwa mujibu wa Sheria.
Saturday, May 06, 2017
Copyright: Dailynews Blog
Mtumie Rafiki Yako
Maoni: 0
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Newer Post
Older Post
Home
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
Tags
Kumbu Kumbu
BUNGE LAPITISHA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LEO
BUNGE limepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 kwa asilimia 73. Bajeti hiyo ambayo ni Shili...
DK KINGWANGALA: KLINIKI YA AFYA YA AKILI KUTOLEWA KUPITIA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA NCHINI
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya viong...
MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YA KUAPISHWA KWA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP
Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo R...
KAJEMBE; MZARAMO ALIYEUTEKA MJI WA MOSHI KWA BIASHARA YA KUKAANGA MIHOGO
WAANDISHI wa Habari ni watu wa kuzunbuka sana nchini na Duniani kwa ujumla katika harakati za utafutaji habari za kuhabarisha jamii juu ...
MREMBO MISS TANZANIA 2003 NARGIS MOHAMED NA GLAMMADAM WAANZISHA DARASA LA UREMBO MTANDAONI
RAIS DKT MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA UTURUKI, WATUBIA MKUTANO WA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA WA NCHI ZAO
Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe wakipokea mashada ya maua kutoka kwa watoto walipowasili Ikulu jijini Da...
TPB BANK YAIPA SERIKALI GAWIO LA BILIONI 1
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akimkabidhi Hundi kifani yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni...
SIKIA USHAURI ALIOPEWA ALI CHOKI KUHUSIANA NA WANAMUZIKI KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
MIILI YA WANAFUNZI 32, WALIMU 2 NA DEREVA WA SHULE YA LUCKY VICENT WALIOKUFA AJALINI YAAGWA
HAKIKA ilikuwa siku ya majonzi makubwa kwa maelfu ya wakazi wa Arusha na viunga vyake pamoja na wale kutoka mikoa mbalimbali ya jirani n...
Labels
BURUDANI
MICHEZO
SIASA
Kumbu Kumbu
January
(86)
February
(95)
March
(131)
April
(117)
May
(113)
June
(127)
July
(81)
August
(69)
September
(46)
October
(55)
November
(21)
December
(47)
January
(66)
February
(32)
March
(41)
April
(40)
May
(27)
June
(9)
October
(1)
BLOG MBALI MBALI
Father Kidevu
SERIKALI KUPITIA MFUMO WA BIASHARA NA UCHIMBAJI WA MADINI YA TANZANITE
MICHUZI BLOG
VETA YAJIWEKEA MKAKATI WA UJUZI KWA VIJANA KATIKA KUWAFUNGULIA FURSA ZA AJIRA
HABARI LEO
Arusha on spotlight
OFA YA MATANGAZO
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment