Rais John Magufuli ameamua kuwa madaktari 258 na wataalamu wa
Afya 11 walioleta maombi na kukidhi vigezo kupitia Wizara ya Afya kwa ajili ya
kwenda kufanya kazi nchini Kenya kuajiriwa na Serikali.
Akifafanua suala hilo Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amesema
makubaliano ya ratiba ya utekelezaji wa ajira hizo za madaktari hao ilikubalika
na pande zote iwe Aprili 6,2017 na Madaktari hao wawe tayari kusafiri
kwenda nchini Kenya kati ya Aprili 6-10 mwaka huu, hadi tarehe ya Taarifa hii
Mahakama nchini Kenya haijaondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu Ajira za
madaktari wa Tanzania nchini Kenya.
Amesema kufuatia uamuzi huu majina ya
Madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika Tovuti ya
Wizara pamoja na wataalamu wengine wa afya 11 walioleta maombi yao na kukidhi
vigezo.
Aidha Serikali ya Tanzania itakuwa tayari
kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa Madaktari 500, pale
ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka madaktari wetu nchini Kenya.
Mnamo tarehe 18 Machi 2017 Ujumbe wa
Serikali ya Kenya ukiongozwa na Waziri wa Afya Dkt.Cleopa Mailu uliwasili
nchini ambapo ulikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John
Pombe Magufuli kwa madhumuni ya kuomba kuajiri kwa Mkataba Madaktari wa
Tanzania mia tano(500) ili kupunguza uhaba wa Madaktari nchini Kenya na
kukubali ombi hilo.
Aidha maombi hayo yalipokelewa ambapo
jumla ya maombi 496 yaliwasilishwa na baada ya kufanya uchambuzi ilibainika
kuwa Madaktari 258 walikidhi vigezo vilivyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini
Kenya.
Lakini wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea kukamilisha utaratibu wa
ajira za Madaktari hao Madaktari watano wa Kenya waliwasilisha pingamizi
mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri Madaktari kutoka
Tanzania.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment