Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano
wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia (pichani) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo kuhusu Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania PLC kutatarajia kupokea maombi mengi ya kununua hisa katika kipindi cha wiki
hii.
Pia kutokana na ushauri kutoka Serikali
ya Tanzania na makundi mbalimbali muhimu ya kijamii yanayohitaji
kuwekeza wakiwemo Wabunge,makundi ya watumishi wa kada mbalimbali wa
serikali na maofisa wa vyama vya Ushirika kutoka sehemu mbalimbali za
nchi,tumewasilisha maombi na kupata idhini kutoka
Mamlaka ya Soko la mitaji na dhamana (CMSA) kuongeza muda wa zoezi la
kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya tarehe
11,Mwezi Mei,2017.
Mkurugenzi huyo alisema kuongezeka kwa muda wa mwisho
wa kununua hisa utawezesha wanaohitaji kununua
hisa kwa makundi binafsi na taasisi zilizoomba muda uongezwe kushiriki
kikamilifu katika mchakato huu.
Tunatoa shukrani za dhati kwa watanzania
ambao wamejitokeza kuwekeza kupitia kununua hisa na tunawakaribisha
ambao bado hawajanunua hisa kuchangamkia fursa
hii katika kipindi cha muda mfupi wa nyongeza.Mgawanyo na mchanganuo wa
umiliki wa hisa inapendekezwa utafanyika kuanzia Mei 19,2017 na
kuendelea kabla ya kumaliza mchakato wa mwisho wa kujisajili katika Soko
la Hisa la Dar es Salaam katika tarehe iliyopangwa
ya Juni 6,2017.”
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment