SERIKALI imesema kuwa imechukua
hatua mahsusi katika kukabiliana
na changamoto zinazotokana na Agenda ya
Mabadiliko ya Umoja wa Ulaya.
Akifafanua hoja hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Suzan Kolimba amesema Serikali imechukua
hatua mbalimbali ambazo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani
na kusimamia matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha tunapunguza utegemezi
kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Pia Serikali inaendelea kuhamasisha sekta
binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa
kuzingatia Sera ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi ya mwaka 2009 na
sheria ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi ya mwaka 2010. Imebainishwa
kuwa mkakati huu unasaidia kuongeza wigo wa vyanzo za fedha za kugharamia
miradi ya maendeleo na kupunguza utegemezi kwa wahisani.
Hata hivyo Serikali inaendelea
kuwashawishi wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza zaidi nchini na
zinaenda sambamba na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara nchini na
kupunguza gharama za kufanya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi
kuwekeza nchini.
Katika kuratibu uhamasishaji wa
watanzania waishio ughaibuni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki imeanzisha Idara maalum ya kuratibu masuala ya Diaspora ili kushiriki
katika Maendeleo ya Nchi ikiwemo kuwekeza nchini.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment