JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA UMMA
ZUIO LA USAFIRISHAJI WA
MAKINIKIA (CONCENTRATES) NA MAWE
YENYE MADINI (ORE) KWENDA NJE YA NCHI
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuujulisha Umma, Kampuni na watu wanaojihusisha
na uvunaji wa madini nchini, kuwa usafirishaji wa makinikia (concentrates) na mawe yeye madini (ore) ya metallic minerals kama vile dhahabu, shaba, nikeli na fedha umesitishwa
kuanzia tarehe 02 Machi, 2017. Usitishwaji huu unalenga kuhakikisha kuwa madini
yanayochimbwa hapa nchini yanaongezewa thamani kabla ya kusafirishwa kwenda nje
hasa kwa ajili ya uyeyushaji (smelting)
na usafishaji (refining) ikiwa ni
utekelezaji wa Sera ya Madini ya Mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.
Aidha, shughuli za uongezaji thamani madini hapa nchini zitatoa fursa ya ajira,
mapato na kuhawilisha teknolojia na hivyo kuleta manufaa zaidi kwa Taifa.
Hivyo, ni mategemeo yetu kuwa Kampuni na watu wote wanaovuna madini
nchini ambao walikuwa wanasafirisha makinikia ya madini pamoja na mawe yenye
madini watazingatia ipasavyo kutosafirisha tena kwenda nje ya nchi kwa ajili ya
uyeyusahji na usafishaji. Wanatakiwa kuanza taratibu za kufanya shughuli hizo
hapa nchini. Serikali itatoa ushirikiano unaotakiwa kwa Kampuni au watu
watakaojishughulisha na shughuli za uchenjuaji madini hapa nchini hasa
uyeyushaji na usafishaji wa madini.
Imetolewa na ;
KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
3 Machi, 2017
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment