Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 9 March 2017

TANESCO YATOA SIKU 14 KWA WADAIWA BILI ZA UMEME KULIPA, VINGINEVYO HUDUMA YA UMEME INASITISHWA


Na Mwandishi Maalum.
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa siku 14 kwa Wateja wake wote linalowadai kulipa madeni yao, vinginevyo litasitisha utoaji wa huduma ya nishati kwa wahusika.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Machi 9, 2017 ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, Shirika linadai jumla ya shilingi Bilioni 275.38.
Akifafanua zaidi alisema, Wizara na Taasisi za Serikali zinadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 52.53, Shirika la Umeme Zanzibar, (ZECO), linadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 127.87, na Makampuni binafsi na wateja wadogo wadogo deni ni zaidi ya Shilingi Bilioni 94.97.
“Zoezi hili litaambatana na utoaji taarifa (notice) kwa wadaiwa wote kulipa madeni yao ndani ya kipindi cha siku 14, baada ya hapo Shirika litachukua hatua ya kusitisha Huduma kwa Wateja watakaoshindwa kuanza kulipa madeni yao pamoja na hatua zingine za kisheria.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Aidha, alisema kwa wale wateja wadogowadogo, Shirika halitawaandikia barua kwani ni wengi, isipokuwa kupitia ofisi ya Uhusiano ya Shirika, wataarifiwa kupitia vyombo vya habari.
Alisema Malimbikizo hayo ya madeni yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya Shirika kwa wakati, ikiwemo shighuli za Uendeshaji Shirika, Matengenezo ya Miundombinu pamoja na utekeelzaji wa miradi mbalimbali.
“Ni matarajio ya Shirika kuwa kuli[wa kwa malimbikizo haya ya madeni, kutasaidia TANESCO kujiendesha kiushindani na kwa ufanisi mkubwa zaidi na hivyo kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme hapa nchini.” Alihitimisha Dkt. Mwinuka.
Taarifa hii ya TANESCO imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuliagiza Shirika hilo, kuwakatia umeme wale wote wanaodaiwa ikiwemo taasisi nyeti za Serikali na hata Zanzibar.
Rais alitoa agizo hilo wakati akizindua ujenzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti 132 mkoani Mtwara ambacho kitaboresha upatikanaji wa umeme kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Baadhi ya viongozi wa TANESCO, kutoka kushoto, Dudu Fuime, (Kaimu Meneja Mwandamizi TEHAMA), Mhandisi Kahitwa Bishaija,(Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji umeme), Mhandisi Theodory Bayona,
(Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme)
  na Renata Ndege, (Afisa Mkuu wa Fedha) wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mkutano huo
Baadhi ya viongoziwa juu wa TANESCO na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Dkt. Mwinuka akiondoka ukumbini baada ya kutoa taarifa hiyo. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha wa TANESCO, Renata Ndege


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment