Wananchi wakishangilia maamuzi ya Rais juu ya utatuzi wa migogoro yao.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Alhaji Majid Mwanga kuwasaka,
kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote wanaodaiwa
kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha
Fukayosi kilichopo Wilayani humo.
Dkt. Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kwenda Jijini Dar es
Salaam ametoa agizo hilo leo tarehe 17 Machi, 2017 aliposimama katika kijiji
hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya
Kata.
Baada
ya kusimamisha msafara wake, Rais Magufuli aliwaita wananchi waliokuwa
wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka
wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe na kisha akatoa nafasi kwa baadhi
yao kueleza dukuduku lao.
Wananchi
hao ambao ni wakulima na mfugaji mmoja aliyejitokeza wakaeleza kuwa Wamang’ati
wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuingiza mifugo katika mashamba yao ya mazao na
wakithubutu kuwakataza wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.
Katika
majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko
wakamatwe Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara
moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji, na
pia kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya
wakulima.
“Kuanzia
leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji
kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia
mimi mwenyewe.
“Kwa
hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili kabla mimi
sijawashughulikia nyinyi, wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na
wafikishwe kwenye vyombo vya sheria” amesema Dkt. Magufuli.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment