Mshindi
wa kundi la Wanawake wa Mashindano ya
Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika Harakati za Mchezo
huo Jana Jijini Dar es Salaam
Mmoja
wa Wachezaji wa Mashindano ya
Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Dkt Edmund
Mndolwa akiwa katika harakati za Mchezo
huo Jana Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance mabeyo akikabidhi Zawadi kwa mshindi
wa Jumla wa Mashindano ya Maadhimisho ya
Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Amani Saidi Jana Jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya Wasanii wa Ngoma kutoka kundi la Ngoma la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Band Coy
wakitumbuiza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu
ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam. /Picha
na Luteni Selemani Semunyu.
***************
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limepania kukuza Mchezo wa Gofu kwa kujenga Miundombinu na Viwanja vya
kanda katika maeneo mbalimbali nchini
kwa Kuanzia Mkoani Dodoma ambapo Serikali imetangaza kuhamia.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati
akifunga Mashindano ya Maadhimisho ya
Miaka 10 tangu Kuanzishwa kwa Klabu ya Golf ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam.
“ Tumeshapata eneo la Jeshi Dodoma hivyo Tutatumia uzoefu
tulioupata kwa Ujenzi wa Klabu hii ili Kujenga Klabu ya Kisasa ya Gofu Mkoani
Dodoma ili watakaokwenda Dodoma kikazi au kwa shughuli nyingine wasikose sehemu
ya Kucheza Gofu.” Alisema Jenerali Mabeyo.
Aliongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Uwanja wa Golf Dodoma lakini pia kuna Uwezekano wa
kujenga Viwanja vya kanda na Lugalo kuwa
na mashina katika Mikoa ya Arusha,Morogoro,Mwanza na Simiyu ili kuchangia
katika ukuzaji wa Michezo na ukizingatia Serikali imetilia Mkazo suala la
Michezo kwa Wananchi.
Jenerali Mabeyo ambaye ni Mlezi wa Klabu hiyo alisema mbali na Ujenzi wa Viwanja hivyo vya
Gofu lakini bado wataendeleza Uwanja wa
Lugalo pale ambapo watangulizi wake wameishia na kuhakikisha unakuwa wenye sifa za
kuchezeka wakati wote kwa kuangalia miundombinu ya Maji.
“ Nilikuwa naongea na mwenyekiti kamati ya mashindano
Dk Edmund Mndolwa alinidokeza tatizo la
kukauka kwa Uwanja kipindi cha Kiangazi na kutochezeka Vizuri nimelichukua na
tutalifanyia kazi tunashukuru Afande
waitara kwa Ubunifu na namshukuru Mtangulizi wangu Jenerali Mwamunyange kwa
kuilea klabu kwa Mafanikio nami kwa
kushirikiana na Wanachama nitaendeleza ili klabu izidi kuimarika”. Alisema
Jenerali Mabeyo.
Pia aliwashukuru Waandishio wa habari na wadau Mbali mbali
katika kuitangaza na kufanikisha
shughuli mbalimbali zinazoandaliwa na Klabu hiyo kwa mafanikio
makubwa na imejidhihirisha kutokana na
Umati mkubwa uliojitokeza katika maadhimisho hayo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia
Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema
katika kipindi cha Miaka 10 wamepata
mafanikio makubwa hivyo sasa licha ya kufanya uwanja kuwa na hadhi ya kimataifa
na mpango maalumu wa ukuzaji vipaji kwa watoton lakini walenga kupata viwanja
kwa ajili ya Michezo mingine ikiwemo kuogelea.
Aliongeza kuwa Lugalo itabaki kitovu cha Ukuzaji vipaji kutokana mpango maalum wa
watoto ambao idadi yao sasa inafikia zaidi ya 50 ambayo ni kubwa ukilinganisha
na Klabu zote nchini.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
mashindano hayo Dkt Edmund Mndolwa alisema wanashukuru JWTZ kwa kutoa
fursa kwa raia kushiriki katika Klabu hiyo hali iliyoondoa adha kubwa
kwa wazalendo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment