Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimuapisha Emanuel
Nchimbi kuwa Balozi Nchini Brazili, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Dkt. James Msekela kuwa Balozi Geneva
–Umoja wa Mataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Mbelwa Kairuki kuwa Balozi nchini China, Ikulu jijini Dar es salaam
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha George Madafa kuwa Balozi nchini Italia
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa
Elizabeth Kiondo kuwa Balozi nchini Uturuki
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Fatma Rajab kuwa balozi nchini Qatar,
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mabalozi wateule wakila kiapo cha Uadilifu
mara baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakwanza kulia ni Balozi Emanuel Nchimbi, Balozi Dkt. James Msekela ,Balozi Mbelwa Kairuki, Balozi George
Madafa, Balozi Prof. Elizabeth Kiondo na Balozi Fatma Rajab
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya
pamoja na Mabalozi wateule mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi mbalimbali aliowaapisha Ikulu
jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU
******************
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo Januari 20, 2017
amewaapisha Mabalozi sita aliowateua jana kuiwakilisha Tanzania katika nchi
mbalimbali.
Hafla ya kuapishwa kwa
Mabalozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mabalozi walioapishwa ni Dkt. Emmanuel John Nchimbi - Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dkt.
James Alex Msekela - Balozi wa Tanzania Geneva - Umoja wa Mataifa, Mbelwa Brighton Kairuki -
Balozi wa Tanzania nchini China,
Fatma Mohamed Rajab -
Balozi wa Tanzania nchini Qatar, George Kahema Madafa - Balozi wa Tanzania
nchini Italy, Prof. Elizabeth Kiango Kiondo – Balozi wa Tanzania nchini
Uturuki.
Wakati huo huo, Kamishna
wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Reginald Nsekela amekula kiapo cha Uadilifu
kwa Viongozi wa Umma mbele ya Rais Dkt.
John Pombe Magufuli.
Baada ya kula kiapo cha
Uadilifu, Jaji Mstaafu Nsekela ameongoza kiapo cha
Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kwa Mabalozi sita walioapishwa leo kwenda
kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.
Akizungumza baada ya
Mabalozi hao kula viapo vyao, Rais Magufuli amewataka kuiwakilisha vizuri
Tanzania katika nchi walizopangiwa kwa kuhakikisha wanasimamia maslai ya
Tanzania.
“Nendeni mkatekeleze
kazi zenu kwa upendo mkubwa mkijua umma wa Watanzania upo nyuma yenu, Maslai ya
Watanzania yakawe mbele, Tanzania kwanza ikawe mbele, na mimi nina uhakika
mtakuwa mmewafanyia Watanzania mema na mazuri sana” “Ukiona kizuri chochote kwa ajili ya
Watanzania kilete, mkatetee Tanzania, mkajenge
uchumi wa Tanzania,
mkaimarishe mahusiano ya Tanzania, mkajenge urafiki wa Watanzania, mkajenge
biashara za Watanzania” amesema Rais Magufuli.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment