Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 24 March 2018

KUWAIT KUING'ARISHA DODOMA KWA BARABARA

Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Dodoma, Machi 23, 2018: Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Balozi Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Aliahidi kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.

Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, Maji na Afya.

Baadhi ya miradi hiyo ambayo imekamilika ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi Somanga inayohusisha pia ujenzi wa Daraja la Mkapa, Kiwanda cha Karatasi Mufindi, Mradi wa kuzalisha Umeme unaotokana na nguvu ya maji-Mtera, na gharama za upembuzi yakinifu wa upanuzi wa Bandari ya Zanzibar.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa Maendeleo wa Kuwait kwa kuisaidia nchi kutimiza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mikopo yenye gharama nafuu inayotolewa na taasisi hiyo.

Dkt. Mpango alisema kuwa mwaka jana, Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait uliipatia Tanzania mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami pamoja na mradi wa maji safi na salama wa miji ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro na sehemu ya eneo la wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wenye thamani ya shilingi bilioni 77,
Mradi mwingine ni ufadhili wa ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar utakaogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.


Wednesday, 21 March 2018

MWANDISHI WA TSN KATUMA MASAMBA AFARIKI DUNIA

MWANDISHI wa habari chipukizi wa vyombo vya habari vya Digital vinavyomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) maarufu kama Daily News Digital, Katuma Masamba (pichani) amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah ilisema Katuma (24) alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam, alikokimbizwa ili kupatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla juzi akishiriki Jukwaa la Biashara la TSN mjini Zanzibar.

Mjomba wa marehemu, Shamte Ally alisema hospitalini hapo jana kuwa mipango ya mazishi ya Katuma ambaye awali alikuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo, itafanyika baada ya kikao cha familia kukaa leo na hasa baada ya mama yake kuwasili.

Dada wa Katuma, ambaye ni mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Nyambona Masamba alisema ndugu wamepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo hicho cha Katuma. 

Taarifa zaidi kuhusu mazishi ya Katuma, zitaendelea kutolewa kwa kadri mipango itakavyokuwa inakwenda. 

Alfajiri ya leo Mjoba wa Marehemu Katuma, Shamte Ally alituma ujumbe mfupi kwa mmoja wa waandishi wa Gazeti tando hili la Daily News Online Blog, Mroki Mroki aliyeko Dodoma na kusema kuwa wanamsubiri mama mzazi wa Katuma anaewasili leo kwa maamuzi juu ya maziko ya mtoto wake.

Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa TSN, wanaungana na familia ya marehemu katika wakati huu mgumu wa maombolezo.


Tuesday, 20 March 2018

MAKONDA AZUNGUMZIA TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA AFISA UBALOZI WA SYRIA.

Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam nimeshtushwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Afisa Ubalozi wa Syria ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha leo mchana Jijini Dar Es Salaam. 

Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe makini zaidi.

Nawaomba sana wananchi wa Dar Es Salaam muendelee kuwa watulivu na mkielewa kwamba Mkoa wenu ni salama salama sana. Vyombo vya usalama vinalifanyia kazi tukio hili na taarifa za awali nilizopokea zinaonyesha tukio hili linaweza kuwa limepangwa na watu wa ndani. Tunafuatilia zaidi kujua kwa nini Afisa huyo hakuomba ulinzi wa polisi akiwa amebeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na pia kwa nini dereva wake amekimbia.

Kwa hali ilivyo mpaka sasa kuna uwezekano ikawa ni tukio la kupangwa na watu wa ndani. Hatutaruhusu watu wachache wachafue taswira ya Mkoa wetu.

Uchunguzi ukifikia sehemu nzuri taarifa rasmi itatolewa na vyombo vyetu vya usalama. Ulinzi na usalama wa wananchi wetu ni muhimu sana.

Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam


MKURUGENZI TBC ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI ILIYOUWA WAWILI KASULU LEO

 Gari la Mkurugenzi wa TBC, Dk Ayoub Rioba STK 8769 likiwa limepinduka baada ya lupata ajali.
Mkurugenzi wa TBC, Dk. Ayub Rioba (kushoto) baada ya ajali hiyo.
                                                                        *******************
WATU wawili wamepoteza maisha huku Mkurugenzi wa Shirika la utangazaji TBC Ayub Rioba amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria STK 8769 kutoka Kibondo kwenda Kigoma mjini kupata ajali katika  Kijiji cha Mgombe Kata ya Nyakitonto Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Akizungumza leo mara baada ya tukio hilo Kamanda wa Polisi Kigoma, Martini Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majinia ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto na Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto ambae hali yake ni mbaya na anendelea naatibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Alisema katika ajali hiyo Waliokuwemo kwenye gari mbali na Dk Rioba ni Mkurugenzi wa Vipindi TBC na Meneja wa Vipindi Kanda ya Magharibi Zabron Mafuru na Dereva aliefahamika kwa jina la Abubakari ambapo wao wamepata majeraha madogo madogo na wamepatiwa matibabu na wanaemdelea vizuri.

Kamanda Otieno alisema Chanzo cha ajari hiyo ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo na kuwaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani. Source: Rhoda Ezekiel -FK Blog Kigoma.


Monday, 19 March 2018

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Sehemu ya Viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Viongozi wa wa taasisi mbali mbali katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Ujumbe wa Umoja wa nchi za Ulaya (EU) katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) .Geoffrey Mwambe,  alipowasili kushiriki katika  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Kulia kwake ni   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel 
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  alipowasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.


MWAKYEMBE ATEMBELEA MAENEO YALIYOTUMIKA KATIKA HARAKATI ZA UKOMBOZI IRINGA

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Chief wa kihehe Evaristo Sambiligunga Mwambeta alipokutana na machief wa kihehe kuzungumza nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Machief wa kihehe (hawapo pichani) alipokutana nao kuzungumzia namna ya kuhifadhi historia ya ukombozi wa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) katika picha ya pamoja na machief wa kihehe baada ya kuzungumza nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akiwasili katika makumbusho ya Mtwa Mkwawa yaliyopo Kalenga kwa ajili ya kuona naoma makumbusho hiyo inavyohifadhi na kuendeleza historia ya shujaa Mkwawa aliyepigana vita vya msituni wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka kwa utumwa wa wajerumani jana Mkoani Iringa. Watatu kulia ni Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akiangalia fuvu la Mtwa Mkwawa alipotembelea makumbusho ya Mkwawa yaliyopo Kalenga kwa ajili ya kuona naoma makumbusho hiyo inavyohifadhi na kuendeleza historia ya shujaa Mkwawa aliyepigana vita vya msituni wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka kwa utumwa wa wajerumani jana Mkoani Iringa.

Mtaalamu kutoka makumbusho  Mkwawa (kulia) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrion Mwakyembe (wapili kulia) baadhi ya vifaa alivyotumia Mtwa Mkwawa wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa ameshika silaha za jadi alizokuwa anatumia Mtwa Mkwawa wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


MPINA ATOA ONYO KALI KWA WATENDEJI WANAOHUJUMU ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA.


 Na John Mapepele, Dodoma
Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa, Luhaga Mpina ametoa onyo kali kwa viongozi wa Serikali katika Halmashauri zote nchini wanayoihujumu operesheni maalum ya kitaifa ya kupiga chapa  mifugo inayoendelea nchi nzima kwa kutoa taarifa za uongo zinazoonesha kuwa mifugo mingi imepigwa chapa tofauti na hali halisi.

Mpina amesema Wizara yake itapita kila Wilaya kufanya tathmini ya kina  baada ya tarehe ya mwisho ya upigaji chapa kitaifa iliyotolewa na Waziri Mkuu, Marchi 31 mwaka  huu ambapo watendaji watakaobainika kudanganya sheria zitachukua mkondo wake.

Aidha ametoa maelekezo kwa Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha kwamba mifugo yote inatakiwa iwe imepigwa chapa hadi tarehe ya mwisho iliyopangwa na kusiwe na visingizio  vyaaina yoyote ikiwa ni utekelezazi wa Sheria ya Utambuzi,Usajili na Ufuatiliaji  wa Mifugo Namba 12 ya Mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011.
Maelekezo hayo  aliyatoa jana akiwa Naibu Waziri wake Mhe. Abdalah Ulega na Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipotembelea mnada wa upili wa Kizota pembeni kidogo wa mji wa Dodoma kutoa tathmini ya zoezi la upigaji chapa nchini kabla ya siku ya mwisho  ya upigaji chapa mifugo yote nchini ambayo ni tarehe 31/3/2018.

Waziri Mpina alisema, kulingana  na takwimu ambazo Wizara imeletewa  hadi Machi 11, 2018 inaonyesha  kwamba,  jumla ya ng’ombe 16,744,355 kati ya 17,390,090 sawa na asilimia 96.3 ya ng’ombe wote nchini wamepigwa chapa. Aidha, jumla ya Punda 51,494 wamepigwa chapa nchini.

“Hivi karibuni nilitembelea mnada wa Pugu nikaangalia idadi ya mifugo iliyopigwa chapa hawafiki hata asilimia tano, lakini leo hapa sote tumeshuhudia idadi ya mifugo wote waliopigwa chapa katika mnada huu wa Kizota ni chini ya asilimia mbili.

Minada hii ndiyo mikubwa nchini ukianzia wa Pugu na huu ni wa Kizota ni wa pili kwa hiyo inadhihirisha kwa uhakika kabisa kuwa kuna udanganyifu mkubwa unaofanywa na watendaji wasio waaminifu wanaopotosha taarifa.” Alisistiza  Mpina

Alisema wilaya nyingine zimeleta takwimu ambazo zinaonyesha zimepia chapa mifugo kwa zaidi ya asilimia elfu moja ambapo amezionya kutojiingiza katika matatizo kwa kuendelea kudanganya.

Aidha alisema tathmini ya jumla kuanzia mwezi Disemba 2017 hadi tarehe 11 Marchi, 2018 inaonyesha kwamba, Halmashauri 85 zimepiga chapa kwa asilimia 100 na zaidi; Halmashauri 86 zimepiga chapa kati ya asilimia 50 na 100, na Halmashauri 4 zimepiga chapa chini ya asilimia 50. 


Saturday, 17 March 2018

MAAFISA HABARI,MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE.

Lango Kuu la Kuingia Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara .
Mkuu wa Idara ya Utalii,Mhifadhi Theodora Aloyce akitoa maelezo kwa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusino Serikalini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara kwa lengo la kutangaza Utalii wa ndani.
Baadhi ya Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakiwa katika gari wakati wa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kujionea vivutio mbalimbali vilivyoko katika Hifadhi hiyo wakiwemo Wanyama mbalimbali.
Miti Mikubwa ya Mibuyu ni sehemu ya Vivutio vilivyoko katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Digi Digi ni mmoja kati ya Wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambaye Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali walipata fursa kumuona.
Mnyama Simba akiwa katika muinuko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ili kumrahisishia kuweza kuona maeneo ya mbali.
Twiga ni miongoni mwa wanyama ambao pia walionekana kwa uzuri zaidi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Baadhi ya Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali wakifurahia ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ikiwa ni pamoja Stori walizokuwa wakipatiwa na waongoza watalii .
Kundi la Swala wakipata malisho ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Tumbili ni miongoni mwa wanyama walioko katika Hifadhi ya Tarangire.
Maafisa Habari wa Taasisi mbalimbali za Serikali wakichukua Taswira katika eneo la Picnic ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Makundi Makubwa ya Tembo ni kivutio kikubwa zaidi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Baada ya Ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara ,Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali wakachukua Taswira  na Mkuu wa Idara ya Utalii katia Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Theodora Aloyce.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YATEMBELEA MGODI WA SEKENKE 1


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Kangi Lugola akisalimiana na Dotto Roman Selasini  Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Iramba mara baada ya kuwasili katika Mgodi wa Senkenke One ulipo katika Kijiji cha Nkonkilangi, Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui, Wilaya ya Iramba akiongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kutembelea mgodi huo kwa lengo la kujionea hali ya mazingira mgodini hapo.



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Kangi Lugola (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Murad SadickA (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Lwehaula wakati wa ziara ya kutembelea mgodi wa Sekenke one Mkoani Singida.



Wabunge wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiangalia zoezi la uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki mara baada ya kutembelea mgodi wa Sekenke one Mkoani Singida.

Wachimbaji wadogo wadogo wa Sekenke one wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais  Kangi Lugola (hayupo pichani) alipopata fursa ya kuzungumza nao na kusisitiza suala la usafi wa mazingira.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Kangi Lugola akifafanua vifungu vya Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kwa watendaji wa Wilaya ya Iramba na kuwataka kuisimamia ili kudhibiti vitendo vya uchafuzi wa Mazingira.