Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday, 5 May 2017

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMEFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI WA MKOA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka  Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakisiliza mafunzo elekezi ya viongozi wa mkoa wa Arusha.
************* 
           
Na Imma Msumba, Arusha
Viongozi wa Mkoa wa Arusha wameshauriwa kuwajibika katika majukumu yao huku wakifuata kanuni na sheria mbalimbali za utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi huku wakileta maendeleo kwa mkoa.
 
Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi hao  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema viongozi wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuongeze mahusiano katika maeneo yao ya kazi baina yao na watumishi wachini yao.
 
Amesema lengo kubwa nikuondoa migongano inayojitokeza baina ya viongozi na watumishi hao ambayo inapelekea kudhorotesha utendaji  wa kazi katika maeneo yao na kuongezeka wimbi la uwonevu kwa watumishi wao.
 
Aidha amewataka viongozi hao wasimamie uwajibikaji wa watumishi katika maeneo ya kazi kwa kufuata taratibu za majukumu yao.
 
Akisisitiza zaidi kwa kuwataka viongozi kutekeleza maelekezo yanayotolewa na ngazi za juu serikalini kwani mengi yanakuwa ni miongoni mwa shughuli zao za kila siku na hii itaongeza utii kwa viongozi serikalini.
 
Nae katibu tawala wa mkoa  Richard  Kwitega amesema mafunzo hayo niyakukumbushana majukumu kwa viongozi hao huku wakipitia maeneo mbalimbali ikiwemo wajibu na majukumu ya viongozi,usimamizi wa Rasilimali watu sehemu za kazi napia kupitia kanuni na maadili ya viongozi na utumishi wa umma.
 
Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku 2 huku yakishirikisha baadhi ya viongozi kutoka TAMISEMI.
Mkuu  wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta wakisikiliza mafunzo ya viongozi wa Mkoa wa Arusha yaliyotolewa kwa lengo lakukuza uwelewa.
Kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Mh: Calist Lazaro pamoja na viongozi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo elekezi kwa viongozi wa mkoa wa Arusha.


WAZIRI MKUU ANUNUA HISA ZA SH MILIONI 20 ZA VODACOM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akielekezwa jinsi ya kujaza fomu  za kununua hisa  za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities,Gerase Kamugisha  (kushoto) wakati alipokuwa akinunua hisa zake na mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani)zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika hafla fupi  iliyofanyika ofisini kwake  jijini Dar es Salaam leo.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji,Bi.Beng’i Issa  na Mkurugenzi  mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikabidhiwa fomu ya kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC   na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities ,Gerase Kamugisha   wakati wa hafla fupi ya kununua hisa zake na mke wake,Mary Majaliwa(hayupo pichani) zenye thamani ya shilingi Milioni 20.Hafla hiyo ilifanyika  ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amenunua hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania Plc zenye thamani ya sh. milioni 10 pamoja na nyingine za sh. milioni 10 kwa ajili ya mke wake, Mary Majaliwa.



Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo leo hii (Ijumaa, Mei 5, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wakuu wa Masoko ya Hisa na Dhamana; Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.



Waziri Mkuu amewasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao. “Hii ni fursa kwa Watanzania kumiliki kampuni. Ukinunua hisa, unashiriki kikamilifu kumiliki kampuni na pia unaboresha uchumi wako binafsi. Ninawasihi Watanzania wote tumieni fursa hii kununua hisa hizo kabla muda haujaisha,” alisisitiza.



Alisema watumishi wa umma wamepewa ya kununua hisa hizo kupitia mipango iliyowekwa na Makatibu Wakuu wao lakini pia amewasihi viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi wachangamkie fursa hiyo ili nchi iweze kupata kodi kupitia makampuni hayo.



“Hii ni fursa kwa kila Mtanzania, kwa viongozi kwa taasisi na mashirika ya umma, taasisi binafsi, wajasiriamali wadogo kama akinamama lishe au madereva wa bodaboda. Watanzania walioko nje ya nchi (Diaspora) nao pia wanunue hisa kwani watakuwa wanachangia uchumi wa nchi na wakati huo wanaweka akiba nyumbani,” aliongeza.



Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango uwekezaji kwenye hisa ni njia mojawapo ya kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi.



“Huko mtaani ukisema uchumi wa nchi unakua, watu wanabisha wakidai kuwa hawaoni unakua kwa sababu hawana fedha mifukoni. Hii ni fursa nyingine ya kuwawezesha kukua kiuchumi, ninaomba waichangamkie,” alisema.



Alisema sekta ya mawasiliano ni miongoni mwa sekta inayokua kwa kasi hapa nchini kwani katika robo tatu ya mwaka, sekta hiyo imekua kwa asilimia 11.3. “Niwasihi Watanzania wenzangu, tununue hisa za Vodacom ili tuweze kuboresha uchumi wetu,” alisema.



Alisema anatoa ombi maalum kwa wafugaji kukubali kuuza mifugo yao na kununua hisa ili kupunguza idadi ya mifugo yao, jambo ambalo alisema litapunguza migogoro baina yao na wakulima.



“Wakulima wa vitunguu, alizeti, maua au wafugaji wa samaki nao pia wanaweza kununua hisa na kuwa na mitaji kwa ajili ya shughuli zao. Ninawasihi wote watumie fursa hii ili kumiliki kampuni,” alisema.



Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana, Bi. Nassama Masinda alisema amefurahishwa kuona Waziri Mkuu akinunua hisa za kampuni ya Vodacom katika soko la awali.



Alisema uuzwaji wa hisa hizo ni utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kuwa wamiliki wa makampuni ya simu za mikononi hapa nchini. “Marekebisho ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta sura ya 306 yanazitaka kampuni za simu na mawasiliano ya kielektroniki kuuza si chini ya asilimia 25 ya hisa zao kwa umma wa Tanzania kupitia masoko ya mitaji (IPO).”



Alisema baada ya hapo hisa hizo zinapaswa kuorodheshwa kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam baada ya kukidhi matakwa ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, sura ya 79. Kampuni ya Vodacom ilitoa hisa milioni 560 kwa umma kwa bei ya sh. 850 kila moja na hivyo kutarajia kukusanya sh. bilioni 476.



Alisema hivi sasa, wawekezaji kwenye masoko ya mitaji ni watu 500,000 tu ikilinganishwa na Kenya ambayo ina wawekezaji milioni 1.7; Uganda (40,000) na Rwanda (14,000). “Vodacom ina wateja milioni 6.2, iwapo nusu ya wateja wake wote watashiriki ununuzi wa hisa, idadi ya wawekezaji kupitia masoko ya mitaji na dhamana itaongezeka kwa asilimia 1,140. Na haya yatakuwa ni mageuzi makubwa katika sekta ya masoko ya mitaji si hapa nchini tu bali katika Afrika Mashariki,” alisema.



Mtendaji Mkuu wa Dodacom, Bw. Ian Ferrao alisema mauzo ya hisa yanayofanywa na kampuni hiyo ni makubwa mara nne ya mauzo ambayo yamewahi kufanyika hapa nchini.



Alisema kampuni hiyo ambayo imekwishafanya kazi kwa miaka 17 hapa nchini, imewekeza zaidi ya sh. trilioni mbili katika mtandao wa mawasiliano nchini Tanzania.


WAZIRI MWAKYEMBE AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YAKE BUNGENI LEO

Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akiwasilisha taarifa ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2017/2018 Bungeni mjini Dodoma leo.
 Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) Dk Jim Yonazi akifuatilia mijadala ya Bunge, Bungeni mjini Dodoma leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Hbari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto mstari wa chini) na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nuru Millao kushoto kwake pamoja na watendaji mbalimbali wa Wizara hiyo wakifuatilia kwa makini mijadala ya Bunge mjini Dodoma jana
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Jamal Malinzi pamoja na wageni wengine wakifuatilia mijadala ya Bunge mjini Dodoma
Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bungeni mjini Dodoma
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akilalamika baada ya kususia kuwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo ya kambi rasmi ya upinzani bungeni mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan ‘Zungu’ akimwelekeza jambo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ baada ya kukiuka kanuni za Bunge wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo ya kambi rasmi ya upinzani bungeni mjini Dodoma
Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Bunge baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini na Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (kushoto) kukiuka kanuni na kususia kuwasilsiah hotuba ya bajeti ya kambi hiyo, Bungeni mjini Dodoma
Wabunge wa Upinzani wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilipokuwa ikiwasilishwa na Waziri Dk Harrison Mwakyembe, Bungeni mjini Dodoma


MWENGE WA UHURU WAKIMBIZWA MADABA

 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari St Getruda iliyopo Halmashauri ya Madaba, Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma wakiulaki mwenge wa uhuru jana,uliofika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa ujumbe wa mwenge kwa mwaka 2017 ambapo kiongozi wa mwenge  kitaifa Amouru Hamad Amour amewataka wanafunzi hao kuhakikisha wanaongeza bidii katika masomo yao ili waweze kufanikisha ndoto walizonazo  kimaisha. Picha zote na Muhidin Amri.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge kushoto,akipokea mwenge wa uhuru jana kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka katika kijiji cha Mahanje halmashauri ya wilaya ya Madaba mara baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake mkoani Njombe
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa  uhuru kwa mwaka 2017, Amour Hamad Amour,akimsikiliza mwenyekiti wa Mahanje Saccos Wilayani Songea, Arika Mgina mara baada ya  kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Saccos hiyo na kupongeza uongozi kwa kazi nzuri inayofanya ya kuwainua  wananchi kiuchumi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Shafi Mpenda, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema.
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017 Amour Hamad Amour akiinua ndoo ya maji jana mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji safi na salama katika kijiji cha Lilondo halmashauri ya wilaya ya Madaba,wakati wa siku ya kwanza ya mbio za mwenge wa uhuru mkoani Ruvuma,kulia ni mkazi wa kijiji hicho Ostella Mwenda.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017 Amour Hamad Amour (kulia) na Mkimbiza mwenge kitaifa Frederick Ndahani wakiomba dua ya kuwaombea waasisi wa mwenge wa uhuru Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Karume katika kijiji cha Lutukira katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba,mara baada ya kukagua kikundi cha vijana waendesha boda boda wanaojishuhulisha na kilimo cha mahindi kijijini hapo.


WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO



Na.Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma
WATANZANIA hususan wale wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano wanatakiwa kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha vyeti  mpya

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati alipofika kupata huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa bungeni hapa.

Waziri Mwijage amesema duniani ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza wananchi wake kwa kuugua ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya zetu,pamoja na kwamba nchi yetu haina mgonjwa wa homa ya manjano.

Aidha amesema maambukizi ya ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake ni ghali sana na inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke reheni maisha yako.

Hata hivyo aliwatahadharisha wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma nje ya nchi ni vyema wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa njia nyingine kwani kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi za kimataifa zina uwezo wa kusoma alama zetu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na vyeti vingi ambavyo vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata chanjo,hivyo ametoa rai kwa  wananchi kuhakikisha wanapata chanjo hizo kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye milipuko wa homa za manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali.

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa kubadilisha vyeti vya zamani hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti vya zamani havitatambulika tena.





TANESCO YAANZA KUWABANA WADAIWA SUGU WA BILI ZA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM

 Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwa na kifaa cha kukatia umeme, tayari kwa kazi kwenye transfoma ya kupeleka umeme kwenye eneo la kiwanda kinachomilikiwa na mfanyabishara maarufu jijini, Bw. Fida Hussein kilichiko Vingunguti leo Mei 4, 2017 


 Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata umeme
 Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara ya fedha TANESCO makao makuu, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mei 4, 2017.
 Mhandisi wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza na waandishi baada ya kusitisha huduma ya umeme kwenye kampuni ya Iprint. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


DC KASESELA ATOA WIKI MBILI KUFANYIKA MIKUTANO YA HADHARA KATA MLANDEGE

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Iringa kama Naibu Meya Joseph Lyata na mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati wakisikiza hoja za wananchi wa Kata ya mlandege.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Watendaji wa kata ya mlandege wamepewe wiki mbili kuitisha mikutano ya kusoma mapato na matumizi ya kila mitaa ili kupunguza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wao.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka viongozi kufanya kazi kwa umakini na kuitisha mikutano ya hadhara kwa wakati ili kupunguza kero zinazowakabili.

"Wananchi wa Kata hii wanakero nyingi ambazo viongozi wa Kata mnaweza kuzitatua sio lazima zinifikie mimi huku,nawaombeni sana viongozi fanyeni kazi la sivyo nitawachukulia hatua mara moja"alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa kata ya mlandege haina changamoto nyingi ili changamoto hizo zinasababishwa na viongozi wa Kata kwa kutofanya mikutano ya hadhara kwa wakati.

Aidha Kasesela alisema kuwa ataendelea kutatua kero zote kwa wananchi kwa kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi na ameletwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kufanya kazi kwa wananchi.

Kero nyingine zilizokuwa hapa Kata ya mlandege zitatatuliwa wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa atazitatuwa kulingana na mipango iliyopo  serikalini.
Kasesela alimuomba mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuzipeleka bungeni baadhi kero ambazo zipo juu ya uwezo wao kama kero ya maji,ardhi na swala Mipangomiji.

Kwa upande wake mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati alisema kuwa ameyapokea na anayapeleka bungeni kuyatatua matatizo na kuyatafutia ufumbuzi wa kero za wananchi.

"Nimekuja hapa kwenye mkutano hadhara kuzichukua kero hizi ili nizipeleke sehemu husika na mimi nitafanya kazi kwa kujituma ili kuisaidia Manispaa ya Iringa kuwa na maendeleo ya haraka sana"alisema Kabati

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa dr mafwele alisema kuwa amezisikia kero zote na atazifanyia kazi kwa umakini mkubwa ili kuboresha maisha ya wananchi wa Manispaa ya Iringa.


Thursday, 4 May 2017

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA TENGERU-SAKINA, ARUSHA

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, bw. Mrisho Gambo. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa maelekezo Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga juu ya upandaji nyasi kwenye eneo la katikati ya barabara wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Cheil Engineering ambayo inajenga barabara ya Sakina-Tengeru, Bw. Shin Pil Soo (wa pili kushoto). Kulia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari na wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa tahadhari juu ya gema lililopo kwenye daraja la mto Ndoruma mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo katika barabra ya kutoka sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto kwake ni Meya wa Arusha, Bw. Calist Lazaro.


Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani Yaadhimishwa Zanzibar

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohmoud Thabit Kombo akipokea maandamano ya Wakunga na Wauguzi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Viongozi wa Wizara ya Afya na Jumiya ya Wakunga, Wauguzi na Wadau wa Afya Tanzania wakati wakipokea maandamano ya Wakunga na Wauguzi katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo Zanzibar.  
Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao
Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao

Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao
MC wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Zanzibar akisoma utaratibu wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar 


Kaimu Msaidizi wa Mrajisi wa Wauguzi na Wakunga Zanzibar Ndg. Rajab Mussa akisoma kiapo cha wauguzi na wakunga wakati wa hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar yalioaza kwa maandamano ya Wakunga na Wauguzi Zanzibar.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakunga Zanzibar Bi Amina Abdulkadir Rajab akizungumza wakati wa maadhimishi ya Siku ya Wakunga Duniani yalioadhimishwa katika ukumbi wa Sanaa rahaleo kwa maandamano yaliopokelewa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
Mwakilishi wa Jumuiya ya Tanzania Midwives Assossiotion Bi Priscilah Godwin akitowa salamu za TAMA wakati wa hafla hiyo ya Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wauguzi Zanzibar Bi Valeria Rashid akitowa salamu za jumuiya yao wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yalioadhimisha Zanzibar katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. 
Rais wa Jumuiya ya CHORA (Construction Health and Relief Acts) Bi Carol Mcdonald akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNFPA Bi Sabina Luoga akitowa salamu za Shirika lake wakati wa maadhimishi ya Siku ya Wakunga Duniani katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar katika hafla hiyo.
Waziri wa Afya Zanzibar akiwahutubia Wauguzi na Wakunga wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani, na kutowa nasaha zake kwa Wauguzi na Wakunga katika utowaji wao wa huduma kwa Mama na watoto, wakati wa kutowa huduza zao katika jamii.   
Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Afya Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani.
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani wakimsikiliza Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohmuod Thabit Kombe akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwa waugunzi na wakunga katika kutowa huduma kwa wananchi wakiwa katika ukumbi wa sanaa rahaleo
Viongozi wa Wakunga na Wauguzi wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani huadhimishwa kila mwezi wa Mei 5, Duniani kote, hafla hiyo ya maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar.