Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 8 April 2018

MANISPAA YA DODOMA WAISHUKURU SERIKALI KUBORESHA ELIMU MSINGI

 

Na Ramadhani Juma,Ofisi ya Mkurugenzi
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imeishukuru Serikali kupitia Wizara ya Elimu kwa kuipatia fedha kwa ajili ya kuimarisha Miundombinu ya Shule mbalimbali za Manispaa hiyo chini ya mradi wa ‘Lipa kwa Matokeo’ maarufu kama ‘P4R’.

Shukrani hizo zimetolewa na Afisa Elimu ya Msingi wa Manispaa ya Dodoma Mwisungi Kigosi alipotembelea Shule mbili za Nkuhungu na Chango’mbe ambazo kila moja inajengewa madarasa mapya nane kwa fedha za mradi huo.
Kwa mujibu wa Kigosi, mradi huo pamoja na mambo mengine, unajenga miundombinu mbalimbali katika Shule sita za Msingi ambapo jumla ya Shilingi milioni 993.1 zinatekeleza kazi hizo.

“Fedha za P4R zina kazi nyingi kama vile kusaidia kukusanya takwimu mbalimbali, kuhamisha Walimu kwa mujibu wa Ikama, na kubwa kabisa ni kujenga miundombinu kama madarasa mapya, kukarabati madarasa ya zamani, na kujenga Vyoo” Alifafanua.
Alisema mradi huo umekuwa mkombozi kwa Shule husika kwa kuongeza na kuimarisha miundombinu kama madarasa kutokana na idadi kubwa ya Wanafunzi inayopelekea upungufu wa madarasa katika baadhi ya Shule.

“Kwa mfano Shule ya Msingi Nkuhungu, mwaka huu wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza ni mia sita…kwa hiyo utaona ni jinsi gani madarasa yanahitajika na hii inatokana na Kata hiyo kuwa na Shule  moja tu ya Serikali” alisema Kigosi. 

Aidha, alizitaja Shule nyingine nne ambako mradi huo unatekelezwa kuwa ni Mahomanyika, Mwenge, Ihumwa, na Nzasa, na kwamba Fedha hizo zimepatikana baada ya Manispaa kukidhi vigezo ikiwemo kuwa na takwimu za uhakika za masuala ya Elimu.Baadhi ya Wanafunzi wa Shule zilizopata Fedha za mradi huo wamepongeza juhudi za Serikali katika kuwatatulia chang’amoto hususani za miundombinu kama vyumba vya Madarasa na Vyoo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment