Rais Dkt. John Magufuli akimuapisha Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018
Rais Dkt. John Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza Dotto Mashaka Biteko akiongea machache baada ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018
Rais Dkt. John Magufuli akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini waliohudhuria kwenye hafla ya kuapishwa . Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018
Rais Dkt. John Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kumuapisha Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018
Rais Dkt. John Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kumuapisha Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018
***********
Rais
Dkt. John Magufuli amemuapisha Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini
na kuiagiza Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha
kanuni za sheria mpya ya madini namba 7 ya mwaka 2017 inasainiwa ifikapo Ijumaa
tarehe 12 Januari, 2018.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya Biteko kuapishwa Ikulu Jijini
Dar es Salaam na ameelezea kutoridhishwa kwake na namna viongozi na watendaji
wa Wizara ya Madini wanavyotekeleza majukumu yao polepole na bila kujali
maslahi ya nchi.
“Sheria
hii imepitishwa na Bunge na mimi nikaisaini tangu mwezi wa 7 mwaka 2017, mpaka
leo ni miezi 7 bado hamjasaini kanuni zake ili sheria ianze kutekelezwa, na
wahusika wote wapo, yaani mpaka leo hamjaelewa Watanzania wanataka nini?
amesema Rais Magufuli.
Amemuagiza
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi kushirikiana na Naibu
Mawaziri, Katibu Mkuu na Wakurugenzi wanaohusika katika Wizara ya Madini
kuhakikisha kanuni hizo zinasainiwa.
Pamoja
na maagizo hayo Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kamishna wa Madini Mhandisi
Benjamin Mchwampaka na amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Kamishna wa
Madini na pia kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini.
Kabla
ya uteuzi huu Prof. Shukrani Elisha Manya alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam Idara ya Jiolojia.
Wakati huo huo,Rais
Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea inafikishwa katika mikoa
yote ya uzalishaji wa chakula ukiwemo mkoa wa Rukwa ifikapo Ijumaa tarehe 12
Januari, 2018.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment