Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho Ijumaa
Oktoba 20, 2017 kwa mchezo mmoja utakaokutanisha timu za Mwadui na
Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga.
Timu
hizo zinakutana katika Raundi ya Saba katika duru hili la kwanza la VPL
ambalo mbali ya Kampuni ya Simu ya Vodacom - wadhamini wakuu, wadhamini
wengine ni Kituo cha Televisheni cha Azam (Azam Tv) na Benki ya KCB
ambayo huduma zake za kibenki zinazidi kushamiri nchini.
Wadhamini
hao wanachagiza ligi hiyo ambayo itaendelea Jumamosi Oktoba 21 kwa
michezo sita itakayofanyika kwenye viwanja tofauti huku mechi nyingi
zikipata fursa ya kuonyeshwa kwenye chaneli mbalimbali za Azam Tv
kupitia king’amuzi cha Azam.
Michezo
ya Jumamosi itakutanisha timu za Mbao na Azam kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza, wakati Lipuli itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya
Songea kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa ilihali Ruvu Shooting
watakuwa wageni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Jumamosi
hiyo hiyo Simba yenye mabadiliko kidogo kwenye benchi la Ufundi,
itawaalika Njombe Mji kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku Ndanda
ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara.
Wakati
Jumamosi hiyohiyo tena, Mtibwa Sugar wakicheza na Tanzania Prisons ya
Mbeya kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, Jumapili kutakuwa na
mchezo mmoja tu - ambao ni kati ya Stand United na mabingwa watetezi,
Young Africans ya Dar es Salaam - mchezo utakaopigwa Uwanja wa Kambarage
mkoani Shinyanga.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment