Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 24 August 2017

WABUNGE WA CANADA WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI.

WABUNGE wa Bunge la Canada ambao pia ni wanachama wa Mabunge ya Jumuia ya Madola  kupitia Mwenyekiti wao Yasmin Rantasi wamepongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

Wabunge hao waliopo katika ziara ya kikazi nchini waliyasema hayo wakati wa kikao maalum baina ya Wabunge hao na Mwenyekiti wa Mabunge ya Jumuia ya Madola Tawi la Tanzania, Dk Raphael Chegeni pamoja na ujumbe wa Bunge la Tanzania, mkutano uliofanyika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

“Tumefurahishwa sana utendaji kazi wa serkali ya awamu ya tano chini ya Rais  Dk. John Magufuli….Uwajibikaji ndani ya serkali umeongezeka, kubana matumizi, vita dhidi ya rushwa na uwekaji wa misingi ya uchumi ni ishara tosha kuwa Tanzania itafanikiwa kukuza uchumi na kupunguza kiwango cha umaskini pamoja na kuboresha huduma za kijamii kwa muda mfupi,” alisema Rantasi.

Rantasi alisema kuwa yeye alizaliwa hapa Tanzania enzi za utawaka wa Mwl. Julius Nyerere na kuondoka akiwa mdogo hivyo kurudi tena katika ardhi hii na kuona maendeleo yanayofikiwa vinampa faraja.
Ujumbe huo unafanya ziara kwa nchi tatu za Afrika zikiwemo Ethiopia, Tanzania na Zambia.

Aidha katika mkutano huo, Dk Chegeni aliwataka wabunge hao kujikita zaidi katika masuala ya kibunge na hasa shughuli na majukumu ya kimsingi ya kibunge ambayo ni  utungaji wa sheria, uwakilishi na usimamizi na ushauri wa serkali zao.

Alisema tawi la Canada lina nafasi kubwa la kuyasaidia matawi mengine ya kibunge kutambua majukumu yakiwemo masuala ya demokrasia, kufuata sheria na kuheshimu utawala wa katiba zao, pia  kutambua utenganifu wa mihimili ya dola.

Katika hatua nyingine, Wabunge hao wamekubali kuanzisha ushirikiano wa kibunge wa moja kwa moja na Bunge la Tanzania ikiwa pamoja na kubadilishana uzoefu, kutembeleana na pia kuhamasisha ushirikiano wa karibu wa serkali hizi mbili.
Pamoja na kikao hicho Dr. Chegeni alisisitiza kuwa hapa Tanzania hakuna raia  aliye juu ya sheria hivyo kila raia anapaswa kuheshimu na kutii sheria ambazo bunge linazitunga.

Sambamba na hilo aliwakumbusha wabunge hao kuendelea kuelimisha wabunge wengine kwa kutumia uzoefu wao na wa mabunge yao njia sahihi za kuheshimu mihili mingine.

“Lengo kuu la wananchi wa Tanzania ni kuendelea kushirikiana na waCanada kupitia serkali zetu ili kuboresha ustawi wa jamii pamoja na kukuza uchumi kwa faida ya watu wa pande  zote,”alisema Dk.Chegeni.

Chegeni ambaye pia ni Mbunge wa Busega, mkoani Simiyu aliwataka wabunge hao kuwahimiza wananchi nchini Canada kutumia vyema rasilimali zilizopo nchini katika uwekezaji kwakua nchi hiyo imejaaliwa teknolojia za kisasa na mitaji ya kutosha.

Rantasi alisema wataendelea kuishauri serkali yao ya Canada izidi kuongeza misaada na kuimarisha uhusiano baina ya serikali hizo mbili kwa maslahi mapana ya mataifa hayo.

Pia walimhakikishia Dk Chegeni kuendelea kushawishi wananchi na makampuni yao kuendelea kutumia fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini kuwekeza zaidi kwani wanaamini Tanzania bado ni nchi yenye utulivu wa kisiasa, inafuata utawala wa sheria na watu wake ni wakarimu.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment