BOFYA VIDEO HIYO KUMSIKILIZA SPIKA WA BUNGE
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai
amesema kuwa wiki ijayo atatoa taarifa kuhusu kazi zilizofanywa na kamati mbili
za wabunge wanaochunguza mwenendo mzima wa makinikia na madini ya vito ili
kuona namna madini hayo yanavyonufaisha Watanzania. Anaandika Francisca Emmanuel
Amesema kuwa licha ya kuwapa
siku 30, kamati hizo bado zinaendelea na kazi na kwamba zilitembelea maeneo ya
machimbo ya madini ikiwemo Merelani kufanya uchunguzi wa kina.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana Dar es Salaam, Ndugai alisema kuwa bunge lililopita la bajeti aliunda
kamati mbili muhimu kufuatilia masuala ya makinikia na madini kwa ujumla hususani
ya dhahabu na kuongeza kamati ya vito (almasi
na Tanzanite) zenye wajumbe 11 kila moja.
‘’Kwa kuwa sikuwepo nchini kwa
wiki kadhaa, itakuwa ni mapema sana kusema
chochote lakini kuanzia kesho kutwa ambapo nitakwenda Dodoma kupata
mrejesho wa shughuli nzima zimeendeleaje lakini taarifa nilizonazo kamati
zimefanya kazi nzuri sana,’’alisema Ndugai.
Alifafanua kuwa wiki ijayo
atatoa taarifa ya nini kitafuata kufuatia kazi za kamati hizo kwani shughuli
kubwa imefanyikia Dodoma.
Hata hivyo, alisema kuwa
kamati nyingine za Bajeti na masuala ya Ukimwi zimeanza vikao vyake na kwamba
Jumatatu kamati zote za Bunge zitaanza vikao Dodoma
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment