Dkt. Kalemani akiongea wakati wa ziara hiyo.
Mhe. Hawa Ghasia akizungumza baada ya ziara ya kutembelea kituo cha kupokea gesi asilia kinachosimamiwa na TPDC.
Wajumbe wa Kamati wakipita pembezoni mwa moja ya mashine kubwa (genereta), kati ya 8 zinazofungwa kwenye mradi wa Kinyerezi II
Hili ndio eneo la upanuzi wa mradi wa umeme Kinyerezi II
Mtandao wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia kutoka kituo cha kupokea gesi hiyo kuelekea eneo la miradi hiyo.
Mafundi wa TPDC wakiwa wamesimama kwenye eneo la utandazaji wa mabomba hayo.
Mhandisi
Manda, (waliyenyoosha mkono), ambaye ni Meneja Mradi wa Kinyerezi II,
akwapatia maelezo wajumbe wa Kamati akiwemo Naibu Waziri Dkt. Kalemani.
*****************
Na
Said Ameir-MAELEZO
Serikali imesema kuwa
viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa matunizi ya gesi
asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza tija tofauti viwanda 37 vya
sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati na
Madini Dk. Medard Kalemani aliiambia Kamati ya Fedha ya Bunge jana kuwa Serikali
imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zinazokwaza zoezi la kuvipatia viwanda
nishati hiyo zinatatuliwa haraka.
“Tuna gesi ya kutosha futi
za ujazo trilioni 57.25 ambapo hadi sasa tunatumia wastani wa futi za ujazo
milioni 70 ikiwa ni kama asilimia kumi tu hivi” alieleza Waziri Kalemani
Kwa hivyo alisema azma ya
Serikali ni kuona viwanda vinatumia gesi katika uzalishaji na kubanisha kuwa Tanzania
inaongoza kwa kuwa na nishati hiyo katika Afrika Mashariki.
Waziri Kalemani aliieleza
kamati hiyo kuwa hivi sasa wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda lakini
Serikali ipo mbioni kutekeleza mkakati wa kusambaza gesi hiyo kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani.
Katika maelezo yake kwa
kamati hiyo ambayo ilitembelea kituo cha kupokelea gesi asilia huko Kinyerezi
na miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi hiyo ya Kinyerezi I na Kinyerezi
II, Naibu Waziri huyo alidokeza kuwa Serikali
ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kusindika gesi asilia ili iweze
kusafirishwa nchi za nje.
Naye Mwenyekiti wa Kamati
ya Fedha ya Bunge Hawa Ghasia ameitaka TPDC kutayarisha mpango maalum kwa
kuainisha na kutenga maeneo maalum ambayo yatawekewa miundombinu ya gesi ili
uwekezaji wa viwanda uzingatie ramani hiyo.
“Tungetengeneza kanda
maalum tukaziandaa kwa ajili ya viwanda kwa kuziwekea miundombinu ya gesi
tofauti na sasa ambapo serikali inalazimika kuvifuata viwanda viliko
kuvipelekea nishati hiyo” alishauri Mwenyekiti huyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti huyo
alieleza kuwa shirika hilo lina nafasi ya pekee katika kuifanya Tanzania
kufikia lengo lake la kuwa nchi ya viwanda kama itatekeleza vyema miradi ya
matumizi ya gesi viwandani.
Aliueleza uongozi wa TPDC
na waandishi wa habari walioambatana katika ziara hiyo kuwa madhumuni ya ziara
ya kamati yake katika miradi hiyo ni kuangalia utayari wa shirika hilo katika
kuchangia maendeleo ya uchumi wa viwanda bila ya vikwazo.
Mwenyekiti huyo alieleza
kuwa kamati yake imeridhika na kazi inayofanyika hadi sasa na kueleza matumiani
ya kamati yake kuwa miradi ya Kinyerezi I na Kinyerezi II itamalizika kwa
wakati na kufikia malengo yaliyowekwa.
Kwa upande wake, Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Kapulya Musomba mpango wa shirika lake sasa ni
kutekeleza programu yake ya kusambza gesi nchi nzima kwa kuanzia na mikoa ya
Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga.
Alisema shirika lake lipo
tayari kukipatia kiwanda au mwekezaji nishati hiyo katika sehemu yeyote ambayo bomba
la gesi hiyo limepita na kwamba ingependeza kuona Tanzania ina viwanda vingi
ili gesi yote iweze kutumika humu nchini pasi na kusafirishwa nchi za nje.
Mapema akijibu maswali
kutoka kwa wajumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Musomba alisema shirika lake linatumia
mifumo miwili ya usalama wa bomba lenye urefu wa kilomita 551 linalosafirisha
gesi kutoka Mtwara hadi eneo hilo.
Aliitaja kuwa ni mfumo
unaojitegemea wa bomba hilo ambapo zinapotokea hitilafu hujizima na wataalamu hufuatilia
kuelewa hitilafu iliopo na mfumo wa pili ni ulinzi shirikishi ambao wanawatumia
wananchi kulinda bomba hilo.
Mbali na viwanda 37 kuunganishwa
katika mfumo wa matumizi ya gesi, shirika hilo pia limeziunganisha familia 70
katika mfumo wa matumizi ya gesi hiyo katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es
salaam.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment