Mkuu wa
Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga akizungumza na ugeni kutoka Benki ya
Kilimo walipomtembelea Ofisi kwake mjini Lindi kuangalia miradi inayoendeshwa
kibiashara mkoani humo.
Mkuu wa
Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya
Kilimo walipomtembelea Ofisi kwake mjini Lindi kuangalia miradi inayoendeshwa
kibiashara mkoani humo.
Maafisa
kutoka Benki ya Kilimo wakifatilia kwa makini mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya
Lindi, Shaibu Ndemanga (hayupo pichani). Kulia ni Afisa Mikopo Mwandamizi,
Mubezi Buberwa na Afisa Usimamizi wa Mikopo, Elizabeth Kitaluta (kushoto).
Meneja wa
Mikopo wa TADB, Samuel Mshote akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu
Ndemanga (hayupo pichani) kuhusu fursa za mikopo inayotolewa na TADB.
***************
Mkuu wa
Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB) kuwasaidia katika kujenga na kuendeleza maghala ili kuwaweza wakulima wa
manispaa hiyo kuhifadhi mazao yao.
Ndemanga
amesema kuwa maghala ya kuhifadhi mazao yamekuwa ni eneo lenye changamoto kubwa
hali inayorudisha nyuma tija kwa wakulima wa manispaa hiyo.
Akizungumza
na ugeni kutoka TADB, uliongozwa na Meneja wa Mikopo wa Benki hiyo, Samuel Mshote,
Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa kutokuwa na maghala ya kutosha katika manispaa kumekuwa kikwazo kikuu kwa wakulima
kufikia malengo yao kwa kuwa imekuwa ikiongoza gharama na upotevu mkubwa wa
mazao yao.
“Changamoto
ya uhaba wa maghala imesababisha manispaa kutokupata mapato stahiki kwa kuwa
uhifadhi wa mazao umekuwa ukifanyika katika maghala ya watu binafsi ambayo
hayakidhi mahitaji halisi ya manispaa,” alisema Ndemanga.
Aliongeza
kuwa ujio wa Benki ya Kilimo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua
changamoto hiyo.
Naye, Meneja
wa Mikopo wa Benki hiyo, Samuel Mshote alisema kwa kutambua changamoto
zinazowakabili wakulima Benki ya Kilimo imeandaa mikopo maalumu kwa ajili ya
kuendeleza miundombinu ikiwemo ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao.
“Mikopo
hii ni kwa ajili ya kujengea miundombinu ya aina mbalimbali kwenye mlolongo wa
thamani, kwa mfano: skimu/ mifumo ya umwagiliaji, maghala ya kisasa ya
kuhifadhia mazao, pamoja na mahitaji mengine ya miundombinu za kilimo,”alisema Mshote.
Kwa mujibu
wa Mshote, mikopo ya aina hii itarejeshwa kwa awamu katika kipindi cha miaka 5
hadi 15.
Akifafanua
zaidi Mshote alisema kuwa ukokotoaji wa marejesho huendana na uwezo wa kuilipa
kwa kuzingatia mpango kazi, na hivyo kipindi kilichoridhiwa kwenye mkataba.
“Tunatambua
kuwa miundombinu ya aina hii, mara nyingi thamani yake huongezeka kadiri muda
unavyopita, miundombinu hiyo huhitaji uangalizi mzuri (maintenance),” alisema.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment