Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 26 August 2017

JENGO LA IMMMA ADVOCATES LILIVYOLIPULIWA NA BOMU USIKU WA LEO


JENGO la kampuni ya Mawakili  wa IMMA  lililopo Upanga jijini Dar es Salaam limevamiwa usiku wa kuamkia leo na kulipuliwa kwa kitu chenye kishindo kikubwa  kinachodhaniwa kuwa ni bomu jambo lililosababisha uharibifu mkubwa   huku kukiwa hakuna kilichochukuliwa. Anaandika Katuma Masamba picha na Mroki Mroki.

Mlipuko huo unadaiwa kutokea majira ya saa 7:30 usiku wa kuamkia jana, na walinzi wawili wa kampuni ya Knight Support iliyokuwa ikilinda jengo hilo wakiokotwa  eneo la Kawe wakiwa hawajitambui.
TSN Digital ilifika eneo la tukio na kuona uharibifu uliosababishwa na mlipuko huo katika jengo la Mawakili hao na jengo la ghorofa nne la Reliance House pamoja na nyumba ya makazi ya Mohammed Ismail.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa  kampuni ya IMMA yenye mawakili 25, Sadock Magai amesema jengo lao  lilitaka kuungua, lakini limeharibiwa   ila bado hawajajua sababu ya watu waliofanya hivyo.
Mbali na Magai Wakurugenzi wenza wanaunda IMMMA ADVOCATES ni pamoja na Protase Ishengoma, Fatma Karume, Faustin Malongo, Gaspar Nyika, Samah Salah na Madina Chenge. 
Amesema uharibifu uliotokea ni mkubwa, ila wakiwa kama Mawakili wenye taaluma hawataki kuhisi sababu za mlipuko huo bali wanasubiri uchunguzi wa Polisi ndio uweze kubaini.

Naye Kaimu Kamanda  Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lucas Mkondya, amesema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuweza kubaini aina ya mlipuko na sababu haswa za kutokea kwa tukio hilo.

Amewataka wananchi na hata wafanyakazi wa jengo  hilo kuwa wavumilivu na kusubiri ripoti ya jeshi hilo kwani askari wako eneo la tukio wakiendelea na uchunguzi.
 Wafanyakazi wakitoka ndani ya jengo hilo.
 Mwandishi wa kujitegemea akipita nje ya jengo hilo.
 Miongoni mwa uharibufu mkubwa uliofanywa na mlipuko huo ni kama huu
 Baadhi ya maeneo yalifukuliwa kuonesha kuwa milipuko ilitegwa ardhini kuteketeza jengo hilo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment