Mtendaji
Mkuu Wa Benki Ya Tpb, Sabasaba Moshingi (Wa Pili Kushoto) Na Kaimu
Mkurugenzi Wa Mfuko Wa Jamii Zanzibar (Zssf) Makame Mwadini Wakitiliana
Saini Makubaliano Ya Kutoa Mikopo Ya Kielimu Na Kuazia Maisha Kwa
Wanachama Wa Zssf, Hafla Hiyo Imefanyika Katika Ukumbi Wa Zssf Kilimani
Mjini Zanzibar. Wakishuhudia Tukio Hilo Ni Afisa Mawasiliano Wa Benki Ya
Tpb Bi. Chichi Banda (Kushoto) Na Afisa Wa Sheria Wa Zssf Bw. Fadhil
Mohammed (Kulia).
Afisa
Mtendaji Mkuu Wa Benki Ya Tpb Bw. Sabasaba Moshingi (Wa Tatu Kushoto)
Na Kaimu Mkurugenzi Wa Mfuko Wa Jamii Zanzibar (Zssf) Makame Mwadini
Wakikabidhiano Mikataba Ya Utoaji Mikopo Ya Kielimu Na Kuanzia Maisha
Kwa Wanachama Wa Zssf, Hafla Hiyo Imefanyika Katika Ukumbi Wa Zssf
Kilimani Mjini Zanzibar. Wakishuhudia Tukio Hilo Ni Wakurugenzi Na
Maofisa Kutoka Benki Ya Tpb Na Mfuko Wa Hidhafi Ya Jamii Zssf.
Makabidhiano Ya Mkataba Wa Makubaliano Baina Ya Benki Ya Tpb Na Zssf.
****************
BENKI
ya TPB imetiliana saini na Mfuko wa Hifadhi Zanzibar (ZSSF), kwa ajili
ya mkopo wa kujikimu na wa elimu ya juu kwa wananchama wa mfuko huo.
Utiaji wa saini ulifanyika jana na kwa upande wa TPB, Afisa Mtendaji
Mkuu, Sabasaba Moshingi aliiwakilisha benki yake na kwa ZSSF
iliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko huo, Makame Mwadini Silima.
Akizungumza
mara baada ya utiaji wa saini hiyo Moshingi, alisema huduma hiyo muhimu
kwa wafanyakazi ambao wanaanza maisha na wale ambao wanataka kuongeza
elimu na kuwataka wanachama wa Mfuko huo kuchangamkia fursa ya mikopo
ili kujiendeleza kimaisha.
Alisema kuwa benki yao itakuwa ikitoa mikopo kwa wanachama hao na baada ya muda watakuwa wakirjesha kwenye mishahara yao.
Alisema
kuwa katika huduma hiyo kila atakayekopa atakaywa riba ya asilimia 12
ya mkopo wake ambayo aliielezea ni ndogo kulingana na aina ya riba ya
mikopo mengine.
Alisema
kuwa huduma hii ya mkopo wa kujikimu na wa elimu ya juu imeanza Dar es
Salaam kupitia Mfuko wa Pensheni wa PSPF pamoja na GEPF na jana ZSSF
walitiliana mkataba baada ya kuona umuhimu wa kuwasaidia wanachama wao.
Kaimu
Mkurugenzi wa ZSSF, Mwadini alisema kuwa hatua hiyo mbali ya
kuwawezesha wananchama wao, itawasaidia kuongeza wanachama wapya kwa
sasa wana wanachama zaidi ya 70,000.
Alisema
kuwa wamefanya mambo mbalimbali ikiwamo kukabiliana na changamoto za
wanachama wao na kuboresha ustawi wa Wazanzibari na Watanzania.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment