Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday, 22 May 2017

WABUNGE WAPEWA SOMO KUHUSU FAIDA ZA UTALII NA UMUHIMU WA KUHIFADHI MAPORI

Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof Alexander Songorwa akitoa mada ya kwanini watanzania tuhifadhi uoto wa asili na wanyamapori wakati wa semina kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa maliasili, malikale na maendeleo ya utalii nchini iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii kwa Wabunge na kufanyika jana Bungeni mjini Dodoma. (Picha na Mroki Mroki).
 Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Serengeti (TAWIRI), Dk. Robert Fyumagwa akitoa mada katika semina hiyo juu ya athari za muingiliano wa mifugo na Wanyamapori.

 Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Prof Dos Santos Silayo akitoa mada juu ya umuhimu wa uhifadhi misitu nchini. 

Profesa Dos Santos Silayo, wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa uhifadhi wa misitu nchini alisema ni vyema misitu ikatunzwa kwa kuwa ndio utajiri mkubwa kwa watanzania.


Alisema misitu ndio huzalisha vyanzo vya maji, husababisha mvua, hutumika kama utalii wa ikolojia, hutunza wanyama na ndege lakini kubwa zaidi husaidia katika kutunza mazingira.
 Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCC), Richard Rugimbana akitoa mada yake juu ya maendeleo ya Utalii na Umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania.
 Maofisa wa Wizara ya Mali Asili na Utalii wakiwa katika semina hiyo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof Alexander Songorwa akitoa mada ya kwanini watanzania tuhifadhi uoto wa asili na wanyamapori. 

Profesa Songorwa endapo uoto wa asili usipohifadhiwa kuna hatari ya kupungua kwa maeneo yaliyohifadhi hewa ya oxygen.

Changamoto nyingine za kutohifadhi uoto wa asili ni kufa kwa mfumo wa ikolojia, wanyamapori na vivutio vya kitalii kuharibika na kupungua na hata kutoweka. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

Mbunge Aida Khenani akifuatilia mada.
 Mbunge wa Mpwapwa, George Malima Lubeleje akisoma moja a majarida ya utalii wakati wa semina hiyo.
 Wabunge wakifuatilia mada katika semina hiyo.
 Meneja mahusiano wa shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Pasco Shelutete akitoa mwongozo katika semina hiyo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akifuatilia mada
 Wanahabari wakifuatailia kwa makini mijadala katika semina hiyo.
 Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika akliachangia.
 Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel akichangia.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanziakifuatilia mijada ya wabunge katika semina hiyo.
 Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akichangia.
 Mbunge wa Muheza, Adadi Mohamed Rajab alikuwa mmoja wa wachangiaji.
 Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akichangia
Mbunge wa Newala Vijijini Ajali Rashid Akibar akichangia


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment