Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene (wapili kulia) akizindua rasmi tawi la DCB benki mjini Dodoma hii leo. Tawi hilo la kwanza la Benki hiyo nje ya jiji la Dar es Salaam na la 10 lipo katika jengo la Mfuko wa LAPF. Kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu, John Samwel Malecela, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DCB Benki, Prof Lucian Msambichaka(wapili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Benki, Edmund Mkwawa
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela akifungua akauinti katika Benki hiyo mjini Dodoma leo huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akimwangalia (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Benki, Edmund Mkwawa akizungumza wakati wa ufunguzi wa tawi hilo jipya na la kwanza la Benji hiyo mjini Dodoma ambapo
alisema kwa sasa benki ina mawakala wapatao 231 waliosambaa Dar es Salaam na
kwaupande wa Dodoma wamefanikiwa kupata
mawakala 38 ambao muda si mrefu wataanza kutoa huduma za DCB mitaa ya Dodoma
karibu zaidi na wananchi.
Waziri Mkuu Mstaafu ambaye ni Mzee Mashuhuri Mjini Dodioma akizungumza wakati wa kutoa neno la ukaribisho na baraka kwa ujio wa Benki ya DCB.
**********
Na
Mroki Mroki-TSN Digital
BENKI
ya DCB imezindua tawi lake la kumi na la kwanza nje ya jiji la Dar es Salaam
hii leo katika Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma.
Akizindua
tawi hilo mjini Dodoma leo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene alipongeza uongozi wa DCB
Banki kwa uamuzi wao wa kufungua twi hilo mjini Dodoma ikiwa ni harakati moja
wapo za kuunga mkono juhudi za serikali kuhamia Dodoma.
Aidha
alisema kufunguliwa kwa tawi hili la Dodoma zitasogezwa huduma za kibenki
karibu na wafanyabishara na wakaazi wa mji wa Dodoma.
“Haya
ndiyo maendeleo tunayotaka katika sekta ya kibenki ili huduma za benki
zipatikane kwa urahisi zaidi kwa wananchi na nina hakika wananchi wengi
watapata huduma bora kupitia tawi hili,” aalisema Waziri Simbachawene.
Waziri
Simbachawene aliwaasa wafanyabiashara, Wafanyakazi na wakazi wote wa mkoani
Dodoma watumie fursa hiyo kwa kufungua akaunti mbalimbali za DCB kupitia tawi
hilo jipya na la kwanza la Benki hiyo nje ya jiji la Dar es Salaam kwa kile
alichoamini kuwa huduma zitakozotolewa na tawi hili zitakuwa bora na zenye
kumjali mteja.
Pia
Waziri huyo wa TAMISEMI aliwaasa viongozi wa Manispaa ya Dodoma kutenga
asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili mfuko wa Wanawake na Vijana na kuingia
mkataba na DCB ili waweze kuratibu utoaji wa mikopo hiyo kwa niaba yao kwa riba
nafuu ya asilimia 10.
“Kwakua
sasa DCB Benki ipo mjini Dodoma na imeonyesha mafanikio makubwa sana ya
uendeshaji na usimamizi wa mikopo hii mkoani Dar es Salaam, nina hakika
itasaidia sana kuwahudumia wajasiriamali wengi mkoani Dodoma,”alisema Waziri
Simbachawene.
Mapema
akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB Banki, Makamu Mwenyekiti wa
Bodi, Prof. Lucian Msambichaka alisema tawi hilo litatoa huduma za kibenki kwa
wakazi, Wafanyabiashara na wafanyakazi wa Dodoma na maeneo jirani.
“Tunatoa
wito kwa wakazi wote wa Dodoma na vitongoji jirani, mtupokee na muwe mstari wa
mbele kutumia huduma za benki tawini hapa ili kukuza tawi hili na kuwa na uwezo
mkubwa wa kuwahudumia wananchi wengi zaidi katika suala zima la kupiga vita
umasikini,”alisema Prof Msambichaka.
Kwaupande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Benki, Edmund Mkwawa, alisema katika kipindi cha
miaka 15 ya utoaji huduma bora, benki hiyo
imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa kuwa karibu zaidi na wateja wake, kubuni
huduma mbalimbali kulingana na matakwa ya wateja kama vile, huduma za kibenki
kupitia mawakala (DCB Jirani) na kupitia
simu ya mkononi (DCB Pesa).
Mkwawa
alisema kwa sasa benki ina mawakala wapatao 231 waliosambaa Dar es Salaam na
kwaupande wa Dodoma wamefanikiwa kupata
mawakala 38 ambao muda si mrefu wataanza kutoa huduma za DCB mitaa ya Dodoma
karibu zaidi na wananchi.
Mbali
na Dodoma, DCB Benki inampango wa kupeleka huduma za DCB mikoa mingine kupitia
DCB Jirani kama vile mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga, Mwanza, Geita, Shinyanga,
Kahama, Mtwara, Arusha, Iringa na Mbeya huku lengo likiwa kuwa na mawakala
1,500 nchi nzima kufikia mwezi Disemba mwaka huu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment