Na Frank Geofray-Jeshi la
Polisi.
Maofisa wakuu wa Polisi wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia
jumatatu tarehe 27-29/03/2017 katika kikao kazi cha siku tatu kujadili na
kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu hapa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa
habari ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Advera
Bulimba alisema kikao hicho kitawakutanisha maofisa wakuu wa makao mkauu ya
Polisi, makamanda wa Polisi wa mikoa na Makamanda wa vikosi bara na Zanzibar
ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utendaji katika
kipindi cha mwaka uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa
mwaka 2017.
Aidha, Bulimba alisema mbali
na utaratibu wa mawasiliano ya kila siku katika kuimarisha usalama wa raia na
mali zao, Jeshi la Polisi pia lina utaratibu wa kukutana kila mwaka kwa pamoja
ili kubadilishana uzoefu kukabiliana na wahalifu kwa lengo la kuhakikisha kuwa
usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika hapa nchini.
“Katika kikao hicho Inspekta
Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu atatoa maelekezo ya kiutendaji ambayo lengo
lake ni kuhakikisha kuwa kila ofisa,
mkaguzi na askari anawajibika kwa nafasi yake katika kuhakikisha uhalifu
unapungua hapa nchini” Alisema Bulimba.
Bulimba alisema kikao kazi
hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu
Nchemba ambapo kauli mbiu katika kikao hicho ni “Zingatia maadili tunapopambana
na uhalifu ili kuimarisha usalama kwa maendeleo ya Taifa”.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment