Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 12 February 2017

RC MTAKA: SIMIYU KUJENGA KIWANDA KIKUBWA CHA BIDHAA ZA AFYA

Na Hamisi Kibari, Simiyu
MKOA wa Simiyu umedhamiria mwaka huu kuanza kujenga kiwanda cha aina yake Afrika Mashariki cha kutengeneza bidhaa za afya zinazotokana na pamba baada ya hatua za upembuzi yakinifu kuelekea kukamilika na michoro ya ramani ya kiwanda kuthibitishwa.

Akiongea jana, siku moja kabla ya Jukwaa la biashara kufanyika mkoani hapa leo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, alisema hatua hiyo, siyo tu kwamba inalenga kutekeleza mpango wa kujenga Tanzania ya viwanda, lakini pia itasaidia katika kuongezea thamani ya zao la pamba. Mkoa wa Simiyu ndio unaotoa asilimia 60 ya pamba yote inayolimwa Tanzania kwa mujibu wa takwimu za mwaka huu.

“Simiyu tunaongoza kwa kuzalisha pamba nchini, lakini unajiuliza tuna sababu gani ya hii nchi kuagiza pamba za kusafisha masikio, tuna sababu gani ya kuagiza bandeji, kuagiza pampasi, kuagiza taulo za usafi wa akina mama, tuna sababu gani ya kuagiza pamba za kusafishia vidonda? Hatuna sababu hiyo,” alisema.

Alisema walikaa na kuona ili wazo la kuanzisha kiwanda hicho kitakachogharimu takribani Sh bilioni 250 lisibaki nadharia wakaamua kushirikisha wadau na sasa linaelekea kuwa kitu halisi.

Mtaka aliyasema hayo wakati akielezea maandalizi ya Jukwaa la Biashara linalofanyika kesho Februari 13,2017 lililoandaliwa na TSN, wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo na Daily News, kwa kushirikiana na Mkoa wa Simiyu, linawakutanisha pia wadau muhimu wa maendeleo kama vile vyombo vya fedha; Benki za TIB na NMB, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
 
Kongamano hilo linatazamiwa pia kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Simuyu kama taasisi mbalimbali zinazoshughulika na biashara au uzalishaji wa bidhaa, masoko, wabunge, halmashauri, wenye viti wa mitaa, wafanyabiashara, wakulima, wawakilishi wa waendesha bodaboda, taasisi za kidini na kadhalika.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment