Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday, 22 January 2018

WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA NYAMIONGO, MWISENGE NA MAKOKO WAPATIWA ELIMU NA MAAFISA KUTOKA OFISI YA BUNGE

Mkurugenzi Msaidizi na Mratibu wa Dawati la Bunge la Afrika kutoka Ofisi ya Bunge, , Lawrence Makigi, akizungumza  jambo wakati akitoa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania kwa Shule za Sekondari za Nyamiongo, Mwisenge na Mokoko ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa elimu kwa Shule za sekondari zilizopo Manispaa ya Musoma, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Manispaa ya Musoma.
Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Nyamiongo, Mwisenge na Mokoko zilizopo Manispaa ya Musoma wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi na Mratibu wa Dawati la Bunge la Afrika kutoka Ofisi ya Bunge,  Lawrence Makigi akizungumza  wakati akitoa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa Elimu kwa Shule za Sekondari zilizopo Manispaa ya Musoma, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Manispaa ya Musoma.
Afisa wa Bunge, kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma,Bakari kishoma akizungumza  wakati akitoa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania kwa Shule za Sekondari za Nyamiongo, Mwisenge na Mokoko ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa elimu kwa Shule za sekondari zilizopo Manispaa ya Musoma, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Manispaa ya Musoma.


Salum Njwete ‘Scorpion’ ahukumiwa jela miaka 7 na faini ya Milioni 30

Na Francisca Emmanuel
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imemuhukumu Mwalimu wa Sanaa ya kujihami, 'Martial arts' Salum Njwete maarufu kama  Scorpion, kutumikia kifungo cha miaka saba jela   na faini ya Sh milioni 30.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ilala, Flora Haule baada ya Scorpion kupatikana na hatia katika kesi ya kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho.

Hata hivyo, mahakama hiyo ilimuachia huru kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Oktoba 31,2017, Mahakama hiyo ilisema Salum Njwete  anakesi ya kujibu ambayo ni Unyanganyi wa kutumia Silaha na kujeruhi.

Scorpion alidaiwa kutenda kosa alilohukumiwa nalo Septemba 6,2016 katika eneo la Buguruni Jijini Dar es Salaam.

Upande wa mashitaka katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi 10 huku Mshitakiwa aliyekuwa akitetewa na Wakili Juma Nassoro alikuwa na mashahidi wawili.


BABU SEYA NA MWANAE WAANZA KUJIFUA RASMI

WAIMBAJI nguli wa muziki wa dance, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanae, Papii Kocha wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.

Wawili hao walipewa msamaha na Rais Dkt John Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji hao wanaopendwa sana kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,Juliana Shonza aliwakutanisha na uongozi wa Wanene Studios waliokubali kuchukua jukumu la kuwarudisha tena kwenye muziki. Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi mpya katika studio hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Wameanza kwa kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni mno kwao kutokana na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.

“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliyamiss, nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” alisema Papii Kocha wakati wa photoshoot.

Kwa kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali zaidi ya zile za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii.


Friday, 19 January 2018

KUTOKA MAGAZETINI LEO JANUARI 18,2018

Pata habari mbalimbali zilizojiri katika Magazeti hii leo. 
BOFYA LINK HII KUPATA UDONDOZI HUO KUTOKA DAILY NEWS DIGITAL


Thursday, 18 January 2018

TANZANIA IMEMALIZA RASMI MUDA WAKE KUONGOZA KUNDI LA G77 NA CHINA KWA MWAKA MMOJA KATIKA UMOJA WA MATAIFA-GENEVA, USWISI

Balozi Dkt. James Alex Msekela akikabidhi uenyekiti wa Kundi la G77 na China Umoja wa Mataifa Geneva kwa Balozi. Farukh Amil wa Pakistani Januari 17, 2017.
Balozi wa Tanzania Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Geneva, UswisiDkt. James Alex Msekela,  akiongoza mkutano wa kukabidhi Uenyekiti wa Kundi la G77 na China Januari 17, 2018 baada ya kuongoza kundi hilo kwa mafanikio makubwa mwaka 2017 ambapo Tanzania ilikuwa Mwenyekiti.
Balozi Dkt. James Alex Msekela akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Mukhisa Kituyi (katikati), Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) na Balozi Amil wa Pakistani wakati wa hafla ya makabidhiano ya uenyekiti wa Kundi la G77 na China, Geneva Uswisi. UNCTAD na kundi la G77 na China zinauhusiano wa kihistoria kutokana na kuwa Shirika hilo lilianzishwa kwa msukumo wa nchi za kundi hilo katika Umoja wa Mataifa kwa lengo la kushughulikia vikwazo vya Biashara, uchumi na maendeleo vinavyokabili nchi zinazoendelea.


RAIS MAGUFULI AMTEUA DK TITUS MWINUKA KUWA MKURUGENZI MKUU TANESCO



Tuesday, 16 January 2018

SERIKALI YAWAPONGEZA WASHINDI WA TUZO ZA KIMATAIFA ZA KISWAHILI YA MABATI -CORNELL YA FASIHI YA AFRIKA 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe,  amewapongeza Dotto Rangimoto na Ali Hilal Ali kwa kushinda tuzo za mashindano ya Kimataifa ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika ya mwaka 2017 yanayoandaliwa na Chuo Kikuu cha Cornell nchini Marekani kwakushirikiana na Kampuni ya ALAF Ltd yaliyofanyika jana Januari15, 2018 mjini Newyork.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa ushindi wa Watanzania hawa ni ushindi wa Taifa kwa ujumla, hivyo kwa niaba ya Serikali anawapongeza sana kwakutangaza utamaduni wetu kupitia lugha ya Kiswahili na kuipeperusha bendara ya Taifa letu Kimataifa. 

Amesema ushindi wa Dotto na  Ali unachagiza juhudi za Serikali za kuibidhaisha lugha ya Kiswahili.

Tuzo za Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika zenye lengo la kutambua na kukuza vipaji vya uandishi kwa lugha za Kiafrika, kuhimiza sanaa ya tafsiri baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe na kutafsiri maandishi ya lugha nyingine kwa lugha za Kiafrika zili asisiwa mwaka 2014. 

Tuzo hizi huandaliwa kila mwaka ambapo washiriki mbalimbali kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki hushiriki. Katika tuzo za mwaka 2017, Dotto Rangimoto ameshinda tuzo katika kipengele cha uandishi wa Ushairi na Ali Hilal Ali ameshinda tuzo katika kipengele cha uandishi wa Riwaya.


RAIS DKT MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI SITA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Nigeria nchini, Sahabu Isah Gada Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Poland nchini,  Krysztof Buzalski Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Uturuki nchini,  Ali Davutoglu Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 16, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Ufaransa mchini,  Frederic Clavier Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Israel hap nchini, Noah Gal Gendler Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Australia nchini,  Alison Chartres Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018.
*****************
RAIS Dkt. John Magufuli leo Januari 16, 2018 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 6 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Sahabu Isah Gada, Balozi wa Poland hapa nchini , Krzysztof Buzalski, Balozi wa Uturuki hapa nchini, Ali Davutoglu, Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Frédéric Clavier, Balozi wa Israel hapa nchini, Noah Gal Gendler na Balozi wa Australia hapa nchini, Alison Chartres.

Akizungumza na Mabalozi hao, Rais Magufuli amewapongeza kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na ameahidi kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati yake na nchi hizo.

Rais Magufuli ametoa wito kwa Mabalozi hao kutilia mkazo ushirikiano katika masuala ya kiuchumi yakiwemo kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo kuja kufanya biashara na kuwekeza hapa nchini, hususani katika viwanda, kilimo, utalii na utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kwamba Serikali itakuwa tayari wakati wote kujenga mazingira bora ya kufanikisha biashara na uwekezaji huo.

Aidha, Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kufikisha salamu zake kwa viongozi wa nchi zao, na kuwakaribisha kuitembelea Tanzania ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano.


MAAFISA HABARI WA SERIKALI KUKUTANA ARUSHA

 Mweyekiti wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) Paschal Shelutete akizungumza kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unatarjiwa kufanyika kuanzia Machi 13, Jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mwenezi wa TAGCO Dkt. Cosmas Mwaisobwa, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus na Katibu Mkuu wa TAGCO Abdul Njaidi.

 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini (TAGCO) na waandishi wa habari kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Katibu Mkuu wa TAGCO Abdul Njaidi na Mweyekiti wa Chama hicho Paschal Shelutete

 Kaimu Katibu Mwenezi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) Dkt. Cosmas Mwaisobwa akisistiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini (TAGCO) na waandishi wa habari kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Katibu Mkuu wa TAGCO, Abdul Njaidi, Mweyekiti wa Chama hicho Paschal Shelutete na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa viongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na MELEZO)