Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday, 30 October 2017

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA: ZINGATIENI VIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA BARABARA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),Elias Kwandikwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,  Aggrey Mwamri, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, alipokagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri,
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,  Aggrey Mwamri,
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akifurahi jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwamri, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ametoa wito kwa madiwani nchini kuanisha barabara zote zenye kipaumbele katika maeneo yao ili ziweze kuingizwa kwa urahisi kwenye mpango wa matengenezo.

Kwandikwa ametoa wito huo mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo yenye urefu wa KM 28 ambapo pamoja na mambo mengine amesema mapendekezo yao yawasilishwe katika kamati za maendeleo za wilaya, mikoa na bodi za barabara.

"Unakuta diwani analalamika kwamba barabara haijatengenezwa ama haifikiliwi kutengenezwa lakini ukija kufuatilia unakuta hakuna mahali popote ambapo taariza za barabara hiyo kutengenezwa zimewasilishwa",    amesema Mhe. Kwandikwa.
Amesisitiza kuwa umuhimu wa kupeleka mapendekezo hayo kutasaidia barabara hizo kutambulika na kuondoa malalamiko kwa wananchi na baadhi ya viongozi kwa kuwa zitaingizwa katika mipango ya ujenzi kwa wakati.

Kuhusu barabara hiyo ya Kaliua-Urambo inayojengwa kufuatia agizo la Rais Dkt John Magufuli, Mhe. Kwandikwa amemtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kwa kuzingatia viwango vya ubora uliopangwa kwa mujibu wa mkataba wake.
"Lengo la mheshimiwa rais ni kurahisha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi hivyo mkandarasi huna budi kufanya kazi hii haraka na kw kuzingatia makubaliano ya mkataba wako.Amesema waziri kwandika.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwamnri, amemuhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa serikali ya mkoa huo imejipanga kushirikiana na mkandarasi ili barabara hiyo ikamilike ndani ya muda uliopangwa.



“Kwanza sisi kama mkoa tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa kutuwekea lami katika barabara hii kwa sababu itaongeza ufanisi kwa wananchi kufanya shughuli zao kiurahisi”, amesema Mwanri.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze amesema kuwa Wakala utawasimamia makandarasi wazawa Samota Construction, Anam Roads Works na Jossam Contractor (JV) ili kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo kwa wakati baada ya changamoto ya tatizo la maji kupatiwa ufumbuzi.

Naibu Waziri Mhe. Elias Kwandikwa, yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.


MAKONDA AMSINDIKIZA RAIS MAGUFULI KWENDA MWANZA LEO


Thursday, 26 October 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU WAKUU, WAKUU WA MIKOA NA MABALOZI

 Mkuu Mpya wa Mkmoa wa Mara, Adam Kigoma Malima
Mkuu wa Zamani wa Jeshi la Polisi Tanzania, Ernest Mangu, aliyeteuliwa kuwa Balozi.
****************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Oktoba, 2017 amefanya mabadiliko katika safi ya Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa kwa kuteua, kupandisha vyeo na kuhamisha vituo vya kazi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameteua amewapandish Naibu Makatibu Wakuu 4 na kuwa Makatibu Wakuu wapya, ameteua Naibu Makatibu Wakuu wapya 7 na amewahamisha vituo vya kazi Makatibu Wakuu 4 na Naibu Katibu Mkuu 1.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 3 na kufanya mabadiliko katika mikoa mingine 3. Na pia amefanya uteuzi wa Balozi mmoja.
Orodha ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo;
1.    Ofisi ya Rais Ikulu.
·      Katibu Mkuu – Bw. Alphayo Kidata

2.    Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
·      Katibu Mkuu (Utumishi)     – Laurian Ndumbaro
·      Naibu Katibu Mkuu            - Dorothy Mwaluko

3.    Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
·      Katibu Mkuu                        - Mhandisi Mussa Iyombe
·      Naibu Katibu Mkuu(Afya) - Dkt. Zainabu Chaula
·      Naibu Katibu Mkuu(Elimu) - Bw. Tixon Nzunda
4.    Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
·      Katibu Mkuu                        - Mhandisi Joseph Kizito Malongo
·      Naibu Katibu Mkuu            - Bi. Butamo Kasuka Phillipo

5.    Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
·      Katibu Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) – Bw. Erick Shitindi
·      Katibu Mkuu(Bunge na Waziri Mkuu) - Maimuna Tarishi
·      Katibu Mkuu(Sera na Uratibu)      - Prof. Faustine Kamuzora